Jumatatu, Julai 07, 2014

JEZI MPYA ZA MANCHESTER UNITED

Manchester United leo wametambulisha uzi wao mpya utakaotumika kwa msimu 2014/15. Straika wa England Wayne Rooney, Robin van Persie na Shinji Kagawa ndio wamewekwa vinara wa utambulisho huo.
Uzi wa juu ukiwa hauna kola umedizainiwa na Nike, michirizi mweupe mikononi na weusi kwa kidogo ndio utakaotumika kwa mara ya kwanza chini ya meneja mpya Louis van Gaal hasa dimbani Old Trafford club.
Kwa wapenzi wa United watakaonunua jezi hizo - kwenye kola watakuta maandishi 'youth, courage and greatness' kumaanisha sera za msimu huu ni 'ujana, ujasiri na mambo makubwa'. Ikimaanisha kwa wachezaji dimbani maneno hayo ndio yatakua muongozo wao dimbani.
Uzi mpya, kikosi kinachojengwa upya na meneja mpya. Nini matarajio yako juu ya klabu hii, umependa jezi gonga like

0 comments:

Chapisha Maoni