
Chanzo chetu cha habari kilisema kwa sasa Lucy anahaha kutafuta cheti feki cha
kipimo hicho kwa kwenda hospitali mbalimbali ili anunue kwa gharama
yoyote lakini imeshindikana.
Ukweli Lucy anahaha kutafuta cheti cha Ukimwi, mchumba anasubiri akione vinginevyo hawatafunga ndoa
kilisema chanzo.
Ilidaiwa kuwa, mpaka sasa Lucy ameshafika kwenye hospitali tatu kubwa
mbili, TMJ na Marie Stopes ili kufanya maarifa lakini imeshindikana.
Baada ya kupata habari hizo tukamtafuta Lucy ambapo alikuwa na haya ya kusema:
Si kweli! Hao wanaosema hivyo ni wanafiki, sijui wanataka nini maana kila siku wanazusha mambo ya ajabu. Kwanza mimi huwa sitibiwagi kwenye hospitali hizo ulizozisema, natibiwa Regency.
Kuhusu kupima Ukimwi, mimi na mchumba wangu tulishapima hukohuko kwao Ulaya (Denmark) ndiyo maana tukaanza taratibu za ndoa.Namshangaa sana huyo aliyesema hayo hata kama ni mtu wangu wa karibu, mimi huwa simwelezi mtu mambo yangu binafsi kwa sababu duniani hakuna rafiki wa kweli, rafiki anakuchekea machoni lakini wote ni wabaya
alisema Lucy.
Amani lilifika kwenye hospitali hizo lakini kukakosekana ushirikiano
kwa madai kwamba, hakuna utaratibu wa kumtaja jina mgonjwa kama
alikwenda kutibiwa.
0 comments:
Chapisha Maoni