Jumatano, Julai 30, 2014

UKATILI MWINGINE, HOUSE GIRL {12} AKATWA MAPANGA NA BOSI WAKE

Msichana wa kazi za ndani, Fonolia Lembres (12) amenusurika kuuawa na mwajiri wake aliyetambulika kwa jina la Emmanuel Msovera ambaye ni kondakta wa Hiace, baada ya kushambuliwa kwa kipigo na kukatwakatwa mapanga mwilini.
Fonolia ambaye kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya Mkoa Mount-Meru, jijini hapa, amejeruhiwa vibaya kwa kukatwa kiganja cha mkono wa kushoto na maeneo mengine ya mwili kisa kikidaiwa kuwa ni kutuhumiwa kuiba shilingi 30,000 za bosi wake huyo.
Hata hivyo, majirani na nyumbani kwa mtuhumiwa huyo wameeleza kuwa msichana huyo amekuwa akipigwa kama mbwa mwitu kila siku kiasi cha wao kumtaka mtuhumiwa amrejeshe kwao iwapo ameshindwa kukaa naye.
Akizungumza kwa tabu akiwa hospitali alikolazwa , mfanyakazi huyo wa ndani alilalamika kutoona vizuri kutokana na jicho lake la kushoto kupigwa ngumi pia maumivu makali ya mkono pamoja na sehemu zingine alizokatwa kwa panga na fyekeo.
Akisimulia tukio hilo alisema, mke wa mtuhumiwa, Rose Benjamini, mumewe alimchukuwa binti huyo kwa wazazi wake miaka minne iliyopita kwa makubalino ya kumsomesha lakini badala yake akawa anampiga mara kwa mara.
Alisema maisha yake yote yamekuwa ya mateso makubwa kwani amekuwa akipigwa na kunyanyaswa kwa kiwango kikubwa na wakati mwingine hata kunyimwa chakula ambapo alikuwa akivumilia mateso hayo.
Alisema siku ya tukio (Jumamosi iliyopita) usiku majira ya saa tatu, Benjamini ambaye ni kondakta wa Hiace zinazofanyakazi kati ya mjini na kwa Morombo, alifika na kumuuliza kuhusu fedha zake kiasi cha shilingi elfu 30 alizoziacha kwenye kochi.
Nilimwambia sikuchukua ndipo alichukuwa panga na kunikata mkono, baadaye alichukuwa fyekeo na kunikata mguuni na sehemu zingine na kunipiga ngumi kwenye jicho
alisema mwanafunzi huyo.
Baadhi ya majirani walioshuhudia tukio hilo walitoa taarifa kwa balozi wa eneo hilo, Joseph Mtinangi ambaye alichukuwa jukumu la kutoa taarifa polisi ambao walifika na kumkuta mtuhumiwa amejifisha
juu ya dari katika chumba chake, wakamkamata na kumfikisha kituo kikuu cha polisi jijini hapa.
Mtuhumiwa huyo amefunguliwa hati ya mashitaka yenye kumbukumbu namba AR/RB/10071/2014 KUJERUHI.Kwa upande wake balozi Mtinangi alilaani tukio hilo na kueleza kuwa ni tukio la kinyama ambalo mtuhumiwa amekuwa akimtendea mara kwa mara msichana huyo.
Aliongeza kuwa alikuwa akipata malalamiko juu ya tukio hilo ambapo aliwaonya wahusika lakini kwa kitendo alichokifanya siku hiyo ametoa wito kwa vyombo vya dola kuchukuwa hatua kali ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.

0 comments:

Chapisha Maoni