Baada ya kuachishwa kazi kutokana na kunywa pombe,
mwanamuziki wa Bendi ya Extra Bongo, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’
amejisalimisha na kuanza kufanya mazoezi na bendi hiyo kwa mara
nyingine.
Mkurugenzi wa bendi hiyo, Ally
Choki alisema Banza alijisalimisha hivi karibuni na kuanza kufanya
mazoezi ya muziki na yeye kama kiongozi hakuweza kumfukuza kwani watu
wengi wamekuwa wakimsihi amrudishe kwani akimuacha ataenda wapi.
Banza ameshakuwa kama mwanangu yaani ni mwanangu hivyo alijisalimisha mwenyewe baada ya kukaa nyumbani kwa muda kutokana na mimi kumtaka asimame kazi kufuatia tabia yake ya kulewa lakini aliporudi sikuona sababu ya kumkataa kwani mashabiki wengi walikuwa wananiambia nimrudishe kwani nikimuacha ataenda wapi? Tuko naye na ninaamini atakuwa amebadilika
alisema Choki.
0 comments:
Chapisha Maoni