MAISHA ya mtoto mwenye umri wa miaka 12, mwanafunzi wa darasa la tano, shule ya
msingi Bwanza (jina tunalo), wilaya ya Bunda mkoani Mara yako hatarini baada ya
samaki aina ya sato kumrukia na kuingia tumboni mwake kwa kupitia sehemu yake
ya siri.
Tukio hilo la aina yake, lililowashangaza wengi kijijini hapo na maeneo mengine jirani, lilimtokea mtoto huyo Januari mosi, mwaka huu, saa 11 alfajiri alipokuwa amechuchumaa akiteka maji ndani ya ziwa Victoria kwa lengo la kumwagilia bustani yao ya nyanya na vitunguu waliyoilima kandokando ya ziwa hilo.
Akiwa amechuchumaa akiteka maji, samaki huyo anayedaiwa kuwa mwenye ukubwa wa nchi nne, aliruka kutoka majini na kumuingia sehemu yake ya siri na kuzama kabisa tumboni mwa mtoto huyo ambaye, jitihada zake za kumvuta ili asizame tumboni hazikufua dafu kwani aliambulia maumivu makali na kutokwa na damu nyingi sehemu yake ya siri kwa kuparazwa na miiba ya mgongoni ya samaki huyo.

Baada ya tukio hilo, alirudi nyumbani kwa shida, akijivuta na kuugulia maumivu makali na kumweleza mama na ndugu zake mkasa uliomkuta ambao, walimchunguza na kujaribu kuingiza mkono sehemu yake ya siri wakidhani watampata samaki huyo lakini hawakufanikiwa.
Kaka wa mtoto huyo, Lenatus Mtani (31) alisema, walipompeleka katika zahanati iliyopo kijijini hapo, hali yake ilizidi kuwa mbaya, akilalamika maumivu makali tumboni, ndipo familia akalihusisha tukio hilo na imani za kishirikina na kuamua kumtoa katika zahanati hiyo na kijijini hapo, na kumpeleka kwa mganga wa kienyeji katika kijiji cha Amuyebe, wilayani Ukerewe.
"Mdogo wangu amechezewa kamchezo, katika hali ya kaawaida samaki hawezi kumrukia mtu sehemu yake ya siri na kuzama tumboni, huu ni ushirikina, tumempeleka kwa mtaalamu lakini bado hali yake inazidi kuwa mbaya" alisema Bw. Mtani
Alisema hata baba yao alifariki katika mazingira ya utatanishi mwaka 2003, kisha kaka zake watatu nao wakafariki kwa mfululizo mwaka 2004, 2005, 2006 wote hao vifo vyao vikigubikwa na utata akidai ni kutokana na ugomvi wa shamba uliopo kati ya familia yao na mkazi mmoja wa kijijini hapo.
Mwenyekiti wa kitongoji cha Alwego anakoishi mtoto huyo, Bi. Reticia Bituro alithibitisha kutokea kwa tukio hilo alilodai limemshutua na kumshangaza sana kwani, hajawahi kushuhudia tukio la namna hiyo tangu azaliwe na kuahidi serikali yake kulifanyia uchunguzi wa kina ili kubaini kama ni mapenzi ya Mungu au kuna mkono wa mtu.
Naye diwani wa eneo hilo la kata ya Napindi Bw. Elias Magoti ambaye yuko safari kuhudhuria kikao cha baraza la madiwani Bunda mjini alikili kupokea taarifa za tukio hilo kwa mshangao mkubwa na kudai atalifuatilia kwa karibu atakaporudi kijijini kwa kufanya uchunguzi kubaini kilichotokea kwani hajawahi kusikia tukio la namna hiyo katika umri wake wote.
Taarifa zilizopatikana kutoka ukerewe anakotibiwa mtoto huyo, zilisema hali yake inazidi kuwa mbaya, hawezi kuzungumza na anazidi kulalamika maumivu makali tumboni ikielezwa kwamba, samaki huyo bado yumo tumboni mwa mtoto huyo.
0 comments:
Chapisha Maoni