Katika taarifa yake iliyotolewa na Kurugenzi ya
Mawasiliano na Uhusiano, chama hicho kimeliomba Jeshi la Polisi kufanya
uchunguzi wa tukio hilo kililoliita kuwa ni la kihuni na mengine ya
namna hiyo yenye lengo ya ukatili dhidi ya binadamu, ili ukweli
ujulikane na haki itendeke kwa sheria kuchukua mkondo wake.
Pia kimewataka wanachama na Watanzania kwa ujumla
kutulia, hasa pale watu wenye hila na malengo yao wanapoanza kukihusisha
na tukio hilo.
0 comments:
Chapisha Maoni