Arsenal imepata pigo baada ya mchezaji wake Theo
Walcott kuthibitishwa kuwa atakosa kushiriki michuano ya Kombe la dunia
kwa kuwa atakuwa kando kwa takriban miezi sita baada ya kupata jeraha la
mguu.
mshambuliaji huyu wa Uingereza mwenye umri wa
miaka 24 alipata jeraha wakati wa michuano ya Kombe la FA siku ya
jumamosi walipokutana na Tottenham na kuichapa mabao 2-0.
Taarifa ya klabu ya Arsenal imesema
Walcott atafanyiwa upasuaji siku zijazo na atakua nje ya dimba kwa
takriban miezi sita ambapo atakosa mechi zote zilizobaki za msimu huu
sambamba na Kombe la dunia.
Michuano ya Kombe la dunia inatarajiwa kuanza
tarehe 12 mwezi Juni, huku Uingereza ikitarajiwa kukipiga na Italia
katika mchezo wake wa kwanza siku mbili baadae.
Rekodi ya Walcott akiwa na Kikosi cha Uingereza.
-Alionekana kwa mara ya kwanza na kikosi cha Uingereza mwaka 2006 ilipocheza na Hungary.
-Alisisimua wengi baada ya kuwa katika kikosi
hicho kwenye Kombe la dunia mwaka 2006 akiwa na umri wa miaka 17 kabla
ya kuingia kwenye ligi kuu nchini Uingereza.
-Aliwahi kufunga mabao matatu dhidi ya Croatia mwezi Septemba mwaka 2008.
-Katika hatua ya kushangaza aliachwa katika kikosi kilichocheza michuano ya kombe la dunia mwaka 2010 nchini Afrika kusini.
Walcott alichukuliwa kutoka Southampton mwaka 2006 kwa kititta cha Pauni milioni 12.5.

0 comments:
Chapisha Maoni