Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi |
MNAMO
TAREHE 06.01.2014 MAJIRA YA SAA 00:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA IGUNDU, KATA YA SANGAMBI, TARAFA YA KIWANJA,
WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. PAUL S/O MWASHEMELE, MIAKA 57, MSAFWA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA
IGUNDU ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU NYUMBANI KWA
NDUGU ZAKE. CHANZO NI BAADA YA KUCHOMWA KISU TUMBONI TAREHE 01.01.2014 MAJIRA YA SAA 12:00HRS
NYUMBANI KWA NGANGA S/O NYAPINI,
MIAKA 48, MSAFWA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA IGUNDU BAADA YA KUMFUMANIA UGONI AKIWA NA MKE WAKE. MAREHEMU
ALIENDELEA KUPATA MATIBABU KWA NDUGU ZAKE MPAKA ALIPOFARIKI DUNIA. MTUHUMIWA
ALIKAMATWA TAREHE 02.01.2014 NA
KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA SHAMBULIO DHIDI YA MKE WAKE AITWAE TUMAIN D/O LUSAMBA,
MIAKA 43, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA
IGUNDU, MTUHUMIWA YUPO GEREZANI RUANDA. KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED. Z. MSANGI ANATOA WITO JAMII
KUACHANA NA TAMAA ZA KIMWILI KWANI ZINA MADHARA MAKUBWA NA BADALA YAKE WATAFUTE
MPENZI MMOJA WA KUISHI NAE.
WILAYA YA MBEYA MJINI –
MAUAJI.
MNAMO
TAREHE 06.01.2014 MAJIRA YA SAA 06:00HRS HUKO KATIKA HOSPITALI YA
RUFAA JIJINI MBEYA, STEPHEN S/O PHILIPO,MIAKA
28,MSAFWA,MKULIMA,MKAZI WA KIJIJI CHA NSUNGWI JUU ALIFARIKI DUNIA WAKATI
ANAENDELEA KUPATIWA MATIBABU. MAREHEMU
ALIPIGWA KITU KIZITO KICHWANI NA KAKA YAKE LUCAS S/O PHILIPO,MIAKA 25, MSAFWA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA NSONGWI
JUU TAREHE 06.01.2014 MAJIRA YA SAA 05:10HRS
HUKO KATIKA KIJIJI CHA NSONGWI JUU KATA
YA NSONGWI, TARAFA YA TEMBELA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI. CHANZO NI UGOMVI WA MASHAMBA BAINA YA WANANDUGU HAO. MTUHUMIWA AMEKAMATWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED. Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUTATUA MIGOGORO YAO YA KIFAMILIA KWA NJIA YA AMANI KWA KUKAA MEZA MOJA YA MAZUNGUMZO ILI KUFIKIA MUAFAKA.
YA NSONGWI, TARAFA YA TEMBELA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI. CHANZO NI UGOMVI WA MASHAMBA BAINA YA WANANDUGU HAO. MTUHUMIWA AMEKAMATWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED. Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUTATUA MIGOGORO YAO YA KIFAMILIA KWA NJIA YA AMANI KWA KUKAA MEZA MOJA YA MAZUNGUMZO ILI KUFIKIA MUAFAKA.
WILAYA YA MBARALI –
AJALI YA GARI KUMGONGA MPANDA BAISKELI NA
KUSABABISHA
KIFO.
MNAMO
TAREHE 06.01.2014 MAJIRA YA SAA 09:45HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA CHAMSALAKA, KATA YA CHIMALA, TARAFA YA ILONGO, BARABARA YA MBEYA/NJOMBE
WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. GARI T.265 BKG AINA YA M/FUSO
BASI LIKIENDESHWA NA DEREVA ZUNDA S/O
ERICK, MBUNGU, MKAZI WA MBEYA
LILIMGONGA MPANDA BAISKELI DAUD S/O
MWAMBENE, MIAKA 53, MNDALI,
MKAZI WA RUAHA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. CHANZO CHA AJALI MWENDO KASI. DEREVA ALIKIMBIAMARA BAADA YA TUKIO
NA KULITELEKEZA GARI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED. Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA
SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO
HILI ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
WILAYA YA MBEYA MJINI –
KUPATIKANA NA NOTI BANDIA.
MNAMO
TAREHE 06.01.2014 MAJIRA YA SAA 21:25HRS HUKO ENEO LA SOKOMATOLA, KATA YA SISIMBA, TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA,
MTU MMOJA AITWAYE MARRY D/O ABRAHAM,
MIAKA 24, KYUSA, MKULIMA NA MKAZI WA SOKOMATOLA ALIKAMATWA AKIWA NA FEDHA
ZIDHANIWAZO KUWA NI BANDIA NOTI 07 @
TSHS 10,000/= ZIKIWA NA THAMANI YA TSHS 70,000/=. MTUHUMIWA ALIKAMATWA BAADA YA KWENDA KWENYE KIBANDA CHA
M-PESA CHA GRACE D/O STEWART, MIAKA
24, KYUSA, MFANYABIASHARA NA MKAZI WA MAJENGO NA KUTAKA KUZIHIFADHI FEDHA HIZO
KWENYE SIMU YAKE. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI AFIKISHWEMAHAKAMANI. KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED. Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
HASA WAFANYABIASHARA KUWA MAKINI NA MATAPELI NA KUENDELEA KUTOA TAARIFA ZA
MTU/WATU WANAOWATILIA MASHAKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAO
ZICHUKULIWE.
[AHMED.Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Chapisha Maoni