Alhamisi, Januari 23, 2014

LULU: NAOGOPA POMBE

Akizungumza na Fichuo Tz hivi karibuni, Lulu alisema tangu ametoka gerezani ameamua kujiweka pembeni na kilevi hicho na kwamba bora aitwe mshamba.
“Kiukweli nikiiona pombe kuna wakati naipa shikamoo kwani ndiyo kichocheo cha kila baya hapa duniani, watakaoniona mshamba kwa kubadilika kwangu wanione hivyohivyo,” alisema Lulu.
Msanii huyo kipindi cha nyumba alikuwa hakamatiki kwa kilevi na kuna wakati aliwahi kuzimika alipofakamia pombe za ofa alipokuwa ndani ya Ukumbi wa Maisha Club, jijini Dar.

0 comments:

Chapisha Maoni