Mahakama kuu kanda ya dar es salaam imeahirisha kutoa maamuzi katika
kesi iliyofunguliwa na mbunge wa Kigoma kaskazini Zitto Kabwe dhidi ya
kamati kuu ya Chadema kwa madai kuwa uamuzi wa mahakama bado
haujakamilika huku kukiwepo ulinzi mkali wa askari wa kikosi cha
kutuliza ghasia FFU ambao walitanda kila kona ya mahakama hiyo.
Ulinzi huo ulimarishwa tangu majira ya asubuhi
ambapo askari hao walikuwa na mabomu ya machozi, silaha za moto mbwa
huku gari la maji ya kuwasha likiwa limeegeshwa pembeni, baada ya
wafuasi wa Zitto na wafuasi wa Chadema kutanda nje ya mahakama hiyo
wakisubiri maamuzi ya mahakama.
Baada ya jaji anayesikiliza kesi hiyo, John Utamwa
kuiahirisha wafuasi hao wakiwa na mabongo yenye ujumbe mbalimbali wakati
wanaondoka eneo hilo la mahakama walinusurika mabomu ya machozi baada
ya kuanza kurushiana mawe na maneno ya kashfa huku wakiimba nyimbo
mbalimbali kama wanavyosikika.
Hali hiyo iliwalazimu askari hao kuanza kupita
wakiwatangazia wafuasi hao watawanyike, watii sheria bila shuruti kabla
hawajachukuwa hatua nyingine zoezi lililochukuwa muda hadi walipoona
askari waliokuwa kwenye pikipiki wanawafuata ndipo wakaanza kukimbia
huku gari lililosheheni askari likiwafuata nyuma.
Mara baada ya kesi hiyo kuahirishwa nje ya mahakama hiyo baadhi ya wafuasi wa Zitto na wafuasi wa Chadema walikuwa na haya.
Zitto alifungua kesi dhidi ya baraza la wadhamini
la Chadema na katibu mkuu, Willibrod Slaa akiiomba mahakama itoe zuio la
muda la kamati kuu kutojadili suala la uanachama wake hadi rufaa yake
itakaposikilizwa na baraza kuu la Chadema,pia aliomba mahakama imwamuru
Dk. Slaa ampe nakala za taarifa za vikao vilivyomvua uongozi ili akate
rufaa.
0 comments:
Chapisha Maoni