Jumatatu, Januari 06, 2014

TUI LA NAZI HUKAUSHA VIRUSI MWILINI

Nazi ikiliwa na binadamu hugeuza aina hizo za mafuta kuwa tindikali ambayo kitaalamu huitwa ‘medium chain fatty acids’ au kwa kifupi (MCFA’s) ambazo huua na kutokomeza virusi vya aina mbalimbali mwilini. Hivyo dawa hii ni chakula na ilitengenezwa maalum kwa waathirika ambao hawana uwezo wa kupata dawa za hospitali ARV’s lakini pia ni nzuri kwa wale ambao wanatumia dawa hizo kwani matokeo ya afya njema hupatikana haraka mno.
Tui la nazi
Matumizi ya nazi kama tiba kwa waathirika wa virusi duniani yalilipuka kwa kasi mwaka 1990 mara baada ya mtafiti wa tiba kutoka Iceland, Bw. Halldor Thormar, kubaini maajabu ya tiba hii.
Waathirika wa virusi vya aina mbalimbali duniani waliotumia nazi walitoa ushuhuda wao wa namna walivyopata nafuu mara baada ya kutumia nazi kama tiba. Licha ya kuponya maradhi waliyokuwa nayo, iliwaboreshea afya zao na kuonekana kana kwamba si waathirika tena.
Dozi yake ni rahisi, unywaji wa glasi nne za tui la nazi kwa siku au vijiko vinne vya mafuta ya nazi kila siku kwa muda wa kati ya miezi mitatu hadi minne, huweza kuondoa maradhi yote yanayosababishwa na virusi mwilini na pia kung’arisha ngozi na kuifanya kuwa nyororo.

Ushahidi wa faida ya nazi kama urembo upo kwa mabinti wa Kizaramo wanaowekwa ndani na kuchuliwa mwili mzima kwa machicha ya nazi kwa miezi kadhaa, ambapo wanapotoka nje huonekana warembo wenye ngozi nyororo waliyoipata kiasili bila kutumia ‘krimu’ au mafuta mengine ya gharama.
Kama sote tujuavyo, virusi vya Ukimwi hudhoofisha kinga ya mwili. Mwili unapokosa kinga hushindwa kuzuia virusi vya aina nyingine kukushambulia. Kwa kawaida tiba ya virusi huwa ni zile dawa zenye uwezo wa kushambulia virusi (antiviral), bakteria (antibiotic) na zile za kushambulia fangasi (antifungus).
Hata hivyo, dawa hizo ni kali sana kiasi cha kuwaumiza watumiaji na huwa na madhara (side effects) zinapotumiwa kwa muda mrefu, ukiachilia mbali gharama zake ambazo mwathirika mwenye kipato cha chini hawezi kuzimudu.
Lakini unaweza kujitibu maradhi yatokanayo na virusi kwa njia rahisi na salama. Kula nazi kwa wingi kadiri uwezavyo, kama ni muathirika basi anza kunywa tui la nazi glasi nne kwa siku na utaona maajabu ndani ya miezi mitatu tu. Kama tayari una vidonda visivyopona basi paka mafuta ya nazi kila utokapo kuoga, na matokeo utayaona bayana.

0 comments:

Chapisha Maoni