Meneja wa bingwa mara saba wa mashindano ya magari ya
langalanga ya F1, Michael Schumacher, ameonya dhidi ya taarifa za
upotoshaji zinazotolewa na baadhi ya watu kuhusu afya ya mwanamichezo
huyo. Onyo hili limekuja baada ya mtu mmoja kukaririwa akisema maisha ya
Schumacher hayako hatarini.
Schumacher bado yuko katika hali "mahututi japo
imara" katika hospitali huko Grenoble nchini Ufaransa baada ya ajali ya
kuanguka na kupigiza kichwa kwenye mwamba wakati akiteleza katika
theluji ya milima ya Alps.
Taarifa kutoka kwa meneja Sabine Kehm imesema
taarifa zote ambazo hazitolewi na mameneja au madaktari, lazima
zichukuliwe kama "uzushi mtupu".
Taarifa hiyo pia imekanusha ripoti ya
kutokabidhiwa kwa hiyari, Camera iliyokuwa imefungwa katika kofia ngumu
"helmet" ya Schumacher wakati wa kuteleza, kuwa hazina ukweli.
0 comments:
Chapisha Maoni