Mwakilishi wa Iran katika Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya
Atomiki (IAEA) amesema katika kikao cha Bodi ya Magavana ya wakala huo
kwamba, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko tayari kuimarisha uhusiano wa
karibu na taasisi hiyo ili kutatua kila aina ya utata uliopo kuhusu
miradi yake ya nyuklia. Redha Najafi pia amesema, Jamhuri ya Kiislamu ya
Iran haitofumbia macho haki yake ya kustafidi na nishati ya atomiki kwa
matumizi ya amani.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhyBYuS3Hn2EShSIJ4nK8Dn1z1xvhOPlf62fj5ec9eamjR32fwAHKhSSxZUJSOYvaNd59TnmEZY_FSfhPINrjP0OhYXvNxmkRv0fR9shhnpVkJuCItighG6S7Alr3G5O5X2b90C1MAQEQOu/s1600/feabe8a9d1bbc8393ad30e845beba7bf_XL.jpg)
Lengo la kwanza la Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (IAEO) ni
kuzalisha umeme yaani kuwa na nishati salama inayotokana na nguvu za
nyuklia.
Katika kufanikisha hilo kiwanda cha kwanza cha atomiki cha Iran
cha Bushehr kilichopo kusini mwa nchi, chenye uwezo wa kuzalisha
Megawati 1000 za umeme wiki ijayo Septemba 24 kitakuwa tayari kwa ajili
ya kukabidhiwa kwa kandarasi wa Kiirani.
Ama lengo la pili la Shirika la
Nishati ya Atomiki la Iran ni kuzalisha fueli kwa ajili ya tanuri yake
ya utafiti ya Tehran sambamba na kulinda mzunguko wa kuzalisha fueli ya
nyuklia.
Hakuna shaka kuwa, kurutubisha urani hakukinzani na sheria za
IAEA wala Mkataba wa NPT, na Iran inataraji kuwa haki yake hiyo
itatambuliwa rasmi na wakala huo. Nchi za Magharibi na zenye kumiliki
fueli ya nyukilia, huku zikiwa na malengo ya upendeleo yamelenga miradi
ya nyuklia ya Iran, na tangu miaka miwili iliyopita yamekataa
kuidhaminia fueli tanuri ya utafiti ya Tehran.
Lakini huku baadhi
wakiamini kuwa, uzalishaji fueli hiyo unahijia miaka isiyopungua miwili
na nusu, wanasayansi wa Kiirani wameweza kufanikisha jambo hilo katika
kipindi cha miezi 18.
Ili kufikia dhumuni hilo la kisayansi, Shirika la
Nishati ya Atomiki la Iran limetekeleza kwa mafanikio awamu ya mwanzo
ya mradi mkubwa wa mzunguko wa fueli nyuklia ambao ni takwa la kitaifa,
kwa kuanzisha kiwanda cha nyuklia cha Isfahan na mradi wa tanuri la maji
mazito huko katika mkoa wa Arak.
Mwaka uliopita pia kulianzishwa
kiwanda cha kurutubisha madini ya urani cha Fordu karibu na mji wa Qum,
ambacho kiko chini ya usimamizi kamili wa IAEA. Hivi sasa fueli
inayotumika katika tanuri ya utafiti ya Tehran imetengenezwa na
wanasayansi wa Kiirani, suala ambalo limeondoa haja ya Iran kuzitegemea
nchi zinazozalisha urani iliyorutubishwa kwa asilimia 20.
Katika ripoti mpya ya Yukia Amano Mkurugenzi Mkuu wa IAEA katika
kikao cha Bodi ya Magavana ilitangazwa kawa, mashinepewa za kizazi kipya
zilizozalishwa ndani ya Iran zinafanya kazi katika viwanda vya nyuklia
hapa nchini.
Hivi sasa aina 15 za dawa za tiba ya mionzi zinazalishwa
nchini Iran na kutumika katika matibabu ya wananchi milioni moja
wanaosumbuliwa na magonjwa ya saratani. Hali kadhalika, ili kuzalisha
fueli inayohitajika katika viwanda vyake zaidi ya 20, inakadiriwa kuwa
Iran inahitaji tani 30 elfu za fueli ya nyuklia suala ambalo
linathibitisha mkakati wa maendeleo ya Iran kwa ajili ya kuzalisha
Megawati zisizopungua 20 elfu za umeme.
Marekani na washirika wake kwa
kutumia vikwazo, mashinikzo ya kisiasa, vitisho vya kijeshi na hata
kuwaua wanasayansi wa nyuklia wa Iran na pia kukwamisha miradi hiyo kwa
kushambulia kwa virusi mitambo ya nyuklia, wanafanya njama za kuzuia
mwenendo wa maendeleo na uvumbuzi katika teknolojia ya nyuklia
inayotumiwa na Iran kwa malengo ya amani.
Lakini licha ya ukwamishaji
huo wa nchi za Magharibi, teknolojia ya nyukilia hii leo ni moja ya
mafanikio muhimu zaidi ya kisayansi yaliyopatikana katika taifa la Iran
0 comments:
Chapisha Maoni