Alhamisi, Oktoba 02, 2014

VITA DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA IRINGA

Wananchi Mkoani Iringa wametakiwa kushirikiana na jeshi la polisi ili kuthibiti ongezeko la vitendo vya uhalifu wa madawa ya kulevya. Kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Iringa ACP Ramadhani Mungi amesema askari polisi wamekuwa wanaendelea na doria ya kuwabaini wauzaji na watumiaji wa madawa ya kulevya ambapo vitendo hivi vimekithiri maeneo ya Makorongoni Manispaa ya Iringa kutokana na kuwa jilani na mjini.
Kamanda Mungi ameongeza kuwa kuna kundi la wafanyabiashara wakubwa wanaowatumia vijana katika biashara hiyo hali inayowaathiri kiafya na kushindwa kushiriki kwenye kazi za uzalishaji mali na kupelekea kujihusisha kwenye vitendo vya ubakaji,kushambuliana na uporaji. Aidha amesema madawa aina ya heloin na cocain ni ya viwandani ambapo uhalifu wa vitendo vya bhangi huongezeka kutokana na kuendelea kwa uzalishaji wake kwa wakulima wa halmashauri za wilaya ya kilolo na Mufindi na mikoa jilani ya Songea na Njombe.
Wakati huo huo kamanda Mungi amesema askari polisi wakiwa doria wamewakamata Vumilia Kihwelo akiwa na bhangi kilo 3 na misokoto 63,Edom Sanga akiwa na bhangi misokoto 21  na Edward Mwambepo akiwa na bhangi kilo 20 wakazi maeneo ya Mjimwema wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa.
Hata hivyo Kamanda Mungi amesema chanzo cha matukio hayo ni kujitafutia kipato hivyo amewaasa wakazi wa Mkoa wa Iringa hasa vijana kujishughulisha na kazi za ujasilia mali zilizo halali kwa jamii.

0 comments:

Chapisha Maoni