CHIPUKIZI wa Bongo Fleva, Ally Timbulo amefunguka kuwa alimwagana na
mwigizaji Skyner Ally ‘Skaina’ kwani aligundua kuwa ana uhusiano na
Mbongo Fleva mwenzake, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’.
Timbulo
alisema ishu hiyo ilitokea miaka kadhaa iliyopita ambapo ‘alimsarendia’
mlimbwende huyo ili awe mpenzi wake na aliposhtuka kuwa ana uhusiano na
Nay wa Mitego, fasta alibadili uelekeo.
“Daah! Nilipogundua ana uhusiano na Nay, fasta nilimpotezea,” alisema
Timbulo, alipotafutwa Skaina, alisema: “Usiniulize hizo habari,
ulivyosikia ndiyo hivyohivyo.”
0 comments:
Chapisha Maoni