
Tukio hilo la kusikitisha lilijiri wiki iliyopita usiku wa manane
Mbagala-Zakhem, Dar, wakati OFM ikiwa katika oparesheni zake kwenye
danguro moja maarufu linalojulikana kwa jina la Kwaswai lililopo maeneo
hayo.
OFM ikishirikiana na polisi wa Kituo cha Mbagala-Kizuiani
ilifumuafumua danguro hilo na kuwanasa watu kadhaa wakifanya vitendo
haramu na hatarishi vya ngono lakini kilichowastaajabisha na kuwaacha
midomo wazi watu waliofurika katika eneo hilo, ni mmoja wa machangu hao
kunaswa akiwa na ujauzito.
Akizungumza na OFM baada ya kuulizwa sababu za kujiuza akiwa katika
hali hiyo, mjamzito huyo alisema hayo yote yanatokana na ugumu wa maisha
kwani alipata mimba akiwa katika kazi hiyohiyo.
Alipoulizwa ujauzito wake una umri gani alidai kuwa bado siku tatu tu itimie miezi tisa akajifungue.
Aliongeza kuwa kwa sasa mmiliki wa danguro hilo amemkataza kujiuza katika danguro lake kwa kuwa angeweza kujisababishia matatizo hivyo aliamua kufanyia biashara zake nje ya danguro hilo.
Aliongeza kuwa kwa sasa mmiliki wa danguro hilo amemkataza kujiuza katika danguro lake kwa kuwa angeweza kujisababishia matatizo hivyo aliamua kufanyia biashara zake nje ya danguro hilo.
“Mbona mnanikamata jamani! Mimi sihusiki na danguro hilo
la...(akimtaja mmiliki) kwanza ameshanikataza kujiuza kwenye danguro
lake kutokana na hali yangu. Yote ni maisha tu jamani!” alisema.
Baadaye Hamisa pamoja na wenzake walipandishwa kwenye karandinga na
kupelekwa kituo cha polisi Mbagala-Kizuiani wakisubiri sheria ichukue
mkondo wake kwani shitaka kubwa linalowakabili ni uzururaji.
0 comments:
Chapisha Maoni