Alhamisi, Oktoba 02, 2014

MATUKIO MAKUBWA MATANO KUTOKA MKOANI MBEYA

KATIKA MSAKO WA KWANZA:

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la shomari athumani (50) mkazi wa mbalizi anashikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa mbeya baada ya kukamatwa akiwa na pombe ya moshi ujazo wa lita 01.
Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 01.10.2014 majira ya saa 17:00 jioni baada ya kufanyika msako huko maeneo ya mapelele, kijiji cha mbalizi, kata ya utengule, tarafa ya bonde la usongwe, wilaya ya mbalizi, mkoa wa mbeya. Mtuhumiwa ni mtumiaji wa pombe hiyo.

KATIKA MSAKO WA PILI:
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la asia jacobo (20) mkazi wa juakali anashikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa mbeya akiwa na pombe haramu ya moshi ujazo wa lita 41/2.
Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 01.10.2014 majira ya saa 17:45 jioni katika msako uliofanyika huko maeneo ya mwanjelwa, kata ya ruanda, tarafa ya iyunga, jiji na mkoa wa mbeya. Mtuhumiwa alikamatwa baada ya kupekuliwa nyumbani kwake. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa pombe hiyo.

KATIKA MSAKO WA TATU:
Watu watano wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa mbeya baada ya kukamatwa wakiwa na pombe ya moshi [gongo] ujazo wa lita wa lita 05. Watuhumiwa hao ni pamoja na 1. Anea songole (45) mkazi wa ilolo 2. Pore amos (28) mkazi wa ilolo 3. Chesco damas (29) mkazi wa mwanjelwa 4. Abdallah kalinga (50) mkazi wa mwanjelwa na 5. Thabiti juma (59) mkazi wa isanga.
Watuhumiwa hao walimakamtwa mnamo tarehe 01.10.2014 majira ya saa 21:30 usiku huko ilolo, kata ya manga, tarafa ya iyunga, jiji na mkoa wa mbeya. Watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa katika klabu cha pombe za kienyeji wakiwa wanakunywa pombe hiyo.
Taratibu za kuwafikisha mahakamani watuhumiwa hao zinaendelea.
Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi ahmed z. Msangi anatoa wito kwa jamii kuacha kutumia pombe haramu ya moshi [gongo] kwani ni hatari kwa afya ya mtumiaji na ni kinyume cha sheria za nchini.

KATIKA MSAKO WA NNE:
Wakazi watatu wa itezi jijini mbeya waliofahamika kwa majina ya 1. Geofrey ndile (32) mfanyabiashara 2. Marina jackson (30) mfanyabiashara na 3. Mashaka mbofu (25) mfanyabiashara wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa mbeya baada ya kukamatwa wakiuza pombe.
Watuhumiwa walikamatwa mnamo tarehe 01.10.2014 majira ya saa 10:00 asubuhi huko itezi, kata ya itezi, tarafa ya iyunga, jiji na mkoa wa mbeya. Watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa wanauza pombe katika klabu cha pombe za kienyeji kiitwacho “jalala” kilichopo itezi. Watuhumiwa wote wamefikishwa mahakama ya mwanzo uyole cc no. 339/2014 na wapo gerezani.

KATIKA MSAKO WA TANO:

Jeshi la polisi mkoa wa mbeya linawashikilia watu wawili waliofahamika kwa majina ya 1. Tanganyika ndelwa (34) mkazi wa ilomba na 2. Selemani nkelaza (34) mkazi wa ilomba baada ya kuwakamata wakinywa pombe kabla ya muda.
Watuhumiwa hao walikamatwa mnamo tarehe 01.10.2014 majira ya saa 11:00 asubuhi huko ccm ilomba, kata ya ilomba, tarafa ya iyunga, jiji na mkoa wa mbeya. Watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa katika klabu cha pombe za kienyeji cha uwanja wa fisi wakinywa pombe kabla ya muda.
Taratibu za kuwafikisha mahakamani watuhumiwa hao zinaendelea.
Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi ahmed z. Msangi anatoa wito kwa jamii kutii sheria bila shuruti, kuacha kunywa/kuuza pombe kabla ya muda uliowekwa kisheria kwani ni kinyume cha sheria.

0 comments:

Chapisha Maoni