SAKATA la kesi ya watangazaji wawili, Ephrahim Kibonde wa Clouds FM
na Gadner G. Habash wa Times Fm wanaokabiliwa na kesi ya kugonga na
kusababisha uharibifu wa gari na kisha kutotii amri ya askari wa usalama
barabarani baada ya kufanya kosa hilo katika eneo la Makumbusho jijini
Dar es Salaam, Agosti 9 mwaka huu, wamefikishwa tena katika Mahakama ya
Kinondoni kujibu mashtaka yanayowakabili.
Wakisomewa mashtaka hayo na mwendesha mashtaka wa serikali, Ramadhan
Mkimbu mbele ya Hakimu Mkazi, Aniceta Wambura alisema washtakiwa
walitenda makosa hayo huku wakijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.
Mshtakiwa wa Kwanza, Eprahim Kibonde anakabiliwa na makosa mawili
ambapo kosa la kwanza ni kuendesha gari huku akiwa amelewa, kosa la pili
ni kugonga gari na baada ya kufanya kosa hilo alikataa kutiii amri ya
Sajent Silvester wakati huo huo, Gadner anakabiliwa na kosa la kutotii
amri na kutoa lugha ya maneno mbele ya askari.
Kesi hiyo imesogezwa mbele hadi Novemba 5 na 21 itakapoanza kutolewa
ushahidi baada ya washtakiwa wote kuiomba mahakama ifanye hivyo kutokana
na mwanasheria anayesikiliza kesi yao kupatwa na dharura.
0 comments:
Chapisha Maoni