Msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amecharukia gari aina ya
BMW 545 alilozawadiwa mwandani wake, Beautiful Onyinye wa Bongo, Wema
Isaac Sepetu ‘Madam’ ambaye ni Miss Tanzania 2006/07, akipinga gari hilo
kupewa na meneja wake, Martin Kadinda.
Habari za kipekepeke zilidai
kuwa, taarifa ya Kadinda kumpa zawadi ya gari Wema kwenye pati ya
bethidei yake Jumapili iliyopita, nyumbani kwake, Kijitonyama, Dar
zilimchanganya Diamond na kudai kwamba ni kitu ambacho hakiwezekani kwa
maana anamfahamu vyema Kadinda kuwa hana uwezo huo wa kununua BMW la
zaidi Sh. milioni 56 za madafu.
Chanzo hicho kiliweka wazi kwamba mkali
huyo anayekimbiza na Ngoma ya Mdogomdogo alihamaki baada ya kupata
taarifa kuwa siyo yeye peke yake aliyekabidhi zawadi ya gari (Nissan
Murano) kwa maana aliamini mwenye zawadi ya gari alikuwa ni yeye tu
ambayo ilikuwa ‘surprise’ kwa mpenzi wake huyo.
Unaambiwa Diamond kachanganyikiwa kabisa kusikia Wema kapewa gari, tena BMW na mbaya zaidi aliyempa gari ni Kadinda huku yeye akiamini kabisa zawadi aliyotoa kwa mpenzi wake asingeweza kupata kwa mtu mwingine yeyote, mwenyewe anasema amedhalilishwa kwani hawezi kutoa gari kisha mwanaume mwenzake naye atoe gari
kilidai chanzo hicho.
Mpashaji huyo alizidi kufafanua kwamba
baada ya kupokea taarifa hizo na kuona kwenye vyombo vya habari na
mitandao mbalimbali akiwa nje ya nchi, Diamond alianza kufanya utaratibu
wa kurudi nchini akitokea Canada ili kujua vizuri kuhusu undani wa hilo
gari.
Yaani ninyi mtasikia, nakwambia kimenuka maana Diamond aliposikia na kusoma habari za BMW la Wema alianza kufanya utaratibu wa kurudi Bongo ili kupata ufafanuzi zaidi
kilisema chanzo hicho.
Kwa upande wake
Kadinda ameendelea kusisitiza kwamba yeye ndiye aliyenunua gari hilo na
kumkabidhi Wema ikiwa ni michango ya watu wanaomsapoti mwanadada huyo.
Kuhusu gari hilo, watu kibao wamekuwa wakitajwa kulinunua akiwemo mfanyabiashara Mkongo mwenye jina linaloanza na herufi S na mume wa mtu ambaye ni kigogo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) jijini Dar anayetajwa kwa herufi moja ya L.Jitihada za kumsikia Wema ziligonga mwamba baada ya simu yake kuita bila kupokelewa na hata alipofuatwa nyumbani kwake hakuwepo hivyo juhudi za kupata lake la moyoni zinaendelea. Stay tuned kwani inavyoonekana nyuma ya pazia ya gari hilo kuna siri kubwa!

0 comments:
Chapisha Maoni