Mtandao wa Facebook umewaomba radhi
jamii ya wanaume na wanawake waliobadili jinsia yao au (transgender) kwa
kusisitiza kuwa lazima watumie majina yao halisi kwenye kurasa sao za
mtandao huo.
Kurasa nyingi za watu wa jamii hiyo zilianikwa au kufichuliwa na mtumiaji mmoja mwezi jana kwa kutumia majina bandia.
Akaunti
hizo, zilisemekana kuwa bandia kwa sababu wamiliki wake walikuwa
wametumia majina yasio yao kama vile, Lil Miss, Hot Mess, badala ya
kutumia majina yao halisi kama vile, Bob Smith kwenye kurasa zao.
Baada
ya pingamizi kutoka kwa watu wa jamii hiyo na jamii nzima ya wapenzi wa
jinsia moja, Facebook kupitia kwa afisaa mkuu wa mauzo Chris Cox,
imetoa taarifa yake na kusema kuwa , itaimarisha sera yake ya ambavyo
watu wanastahili kujitambulisha kwenye mtandao wa Facebook katika kurasa
au akaunti zao.
Nataka kuwaomba radhi wale wote waliohisi kutendewa ubaya kutokana na sakata hii.Hii ni kwa sababu Facebook inataka watu watumie majina yao halisi wala sio utambulisho bandia.
Hata hivyo.
Watu hao walikuwa wametishia kuondoka kwenye mtandao huo na kuandaa maandamano makubwa mjini San Francisco.
Msemaji wa watu wa jamii hiyo,Mark Snyder, alisema wameridhika baada ya Facebook kuwaomba radhi.
Alisema
kuwa sio watu wa jamii hiyo pekee wanaotaka kutumia majina ambayo sio
yao ili kujilinda kutokana na kejeli kwenye mitandao.
Hata hivyo
Facebook imekuwa ikisisitiza kuwa watumiaji wa Facebook sharti watumie
majina yao halisi ili wapeukane na kejeli kwenye mtandao pamoja na watu
kutumia majina yao.
0 comments:
Chapisha Maoni