Alhamisi, Oktoba 23, 2014

IRINGA NA DAFTARI LA WAKAZI

Wananchi wa mkoa wa Manispaa ya Iringa Mkoani Iringa wametakiwa kuendelea kushiriki kwenye daftari la wakazi litakalo malizika Octobrer 30 mwaka huu.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Mkoani Iringa Bi.Theresia Mahongo amesema zoezi la uandikishaji kwenye daftari la wakazi lilianzishwa chini ya sheria ya serikali za mitaa ya mwaka 1982,likiwa na taarifa za kuhama,uhamiaji pamoja na taarifa za kuzaliwa kwa watoto wa mtaa husika.
Akizungumza na Fichuo Tz, bi.Mahongo ameongeza kuwa dafari hizo husaidia kutambua idadi ya wakazi,uandaaji wa mipango ya manispaa kwenye nyanza mbaimbali,ulinzi na usalama na upatikanaji wa vitambulisho vya taifa vinavyoandaliwa na mamlaka ya vitambulisho vya taifa NIDA.
Aidha amesema viongozi wanaohusika na usimamizi wa zoezi hili ni watendaji wa mitaa wakisaidiana na wenyeviti wa mitaa ambao wanawafahamu wakazi wao na ambao wanatambulika katika mfumo wa serikali kwenwe ngazi a mtaa.
Hata hivyo Bi.Mahongo amesema zoezi hili limekuwepo kwa mda mrefu ila wananchi wamekuwa hawaingizi taarifa zao katika daftati hilo na na baadhi yao hawajui uwepo wa zoezi hilo pia ametoa wito kwa wananchi kuto changanya  uandikishaji wa madaftari ya vyama wenye lengo la kujua idadi ya wanachama wao.

0 comments:

Chapisha Maoni