Alhamisi, Oktoba 23, 2014

SHYROSE BHANJI AZUA BALAA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI

Shyrose Bhanji kazua balaa kwenye Bunge la EAC huko Kigali jana na leo! Walioandika trh 8 kwenda Brussels kwenye Bunge la EU members wote wa Tume yao na Wenyeviti wa Kamati. Wakiwa safarini kwenda ndani ya ndege sijuwi kukosa ile lishe aliyoizoea? Akawa anakunywa kama kichaa! Crews wakamzuia kuwa kwakuwa ndege ni ya mchana asinywe kupitiliza. Akaanza kutukana crews matusi yote unayoyajua! 
Akawaambia hawajuwi kama yeye ni mbunge wa EAC? Akaanza kufanya fujo ndani ya ndege, akachukua chupa akapasua! Hapa security ndani ya ndege wakamkamata na kumtia pingu! Maneno yakawa yanamtoka ovyo. Wenzie walipojaribu kumtuliza wa kutoka Rwanda na mwingine Uganda (names withheld) akawageukia, tukana hadi marais wao hya kutosha! Hapo walikuwa juu ya anga ya Cairo.
Pilot akakataa kuendelea na safari akataka kushusha ndege Cairo. Walimsihi sana Pilot ndio akakubali kwa masharti Shyrose adhibitiwe!
Walipofika Brussels vituko havikuishia hapo. Kwenye mikutano anabwabwaja ovyo. Mbaya zaidi akaandika ki-note na kukiweka mgongoni ili walio row ya nyuma yake wakisome. Kiliandikwa kuhusu yule mbunge/Waziri wa EAC aliyefariki kuwa amekufa kwa UKIMWI, na kwa kuwa amelala na Wabunge wanawake wa EALA (kawaandika majina kwenye ki-note) nao wana UKIMWI kwa kuwa wanaumwa mara kwa mara.
Wakamaliza ziara ambayo hata Spika wa EALA alikuwepo, Wabunge toka Tz waliokuwepo pamoja na Shyrose ni Kimbisa na Angella Kizigha; kwa rekodi mbaya!
Sasa Bunge la EALA limeanza vikao juzi, jana Bunge limevunjika, hawataki kujadili Miswada wala nini hadi Shyrose ajadiliwe Bungeni kwa mambo ya aibu aliyoyafanya ktk ziara hiyo. Bunge likavunjika!
 Leo asbh kulikuwa na kikao cha House Business, ambacho kwa huku Bongo ni kama Kamati ya uongozi. Agenda ni Shyrose na kuvunjika kwa Bunge jana. Kikao kimevunjika na Wajumbe wote wamejiuzulu! Wanasema kwanini Spika hakumkemea Shyrose alipofanya ujinga kwenye ndege? Kwanini hamuwajibishi kwa kumfukuza Bungeni ilhali anajua sifa zote mbaya za Shyrose tangu ameingia EALA? Sasa hivi wote wamejiuzulu na sasa si tu wanataka Shyrose afukuzwe bali na Spika ajiuzulu mara moja!
Wajumbe wanadai walipojitoa na kujiuzulu, Spika peke yake hajajitoa, hivyo naye aende na maji! Yaani hakuna kinachoendelea, Wabunge wanasema Bunge halitaendelea wala kufanyika hata kwa miaka 10 ijayo hadi Shyrose na Spika waondoke!
Hii ni aibu kubwa kwa nchi yetu! Kila Shyrose anapopita hukosi kusikia kapigana, kagombana, katukana au kufanya mambo ya aibu! Hapo EALA kagombana na watu wengi kuanzia Wabunge wenzie hadi staff.

0 comments:

Chapisha Maoni