Jumatatu, Juni 09, 2014

MFAHAMU ALIYETUNGA JINA LA TANZANIA, ANAITWA MOHAMED IQBAL DAR

Katika kumbukumbu muhimu nimeona niwakumbushe na kuwafahamisha jambo zito kwa wale wasiojua.
 Nianze na swali je, unamjua huyu mtu aliyetunga jina la Tanzania? Bila shaka wengi hawajui kwa sababu hili huwa haliandikwi au kutangazwa kwa sababu ambazo mimi sizijui.
Kumbukumbu zinasema mtu huyu aliyebuni jina la Tanzania anaishi mkoani Mtwara.
Kumbuka jina la Tanzania lilibuniwa baada ya kuunganishwa nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar Aprili 26, mwaka 1964  kwa kuchanganywa udongo wa nchi hizo na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyekuwa Rais wa Tanganyika na Sheikh Abeid Amani Karume aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar.
Huyu bwana aliyebuni jina la Tanzania ni Mtanzania mwenye asili ya Kihindi na dini yake ni Ahmadiya Muslim Jamaat Tanzania na majina yake ni Mohammed Iqbal Dar (pichani).
Mohammed alizaliwa mkoani Tanga mwaka 1944. Baba mzazi wa Mohammed alikuwa daktari mkoani Morogoro alikuwa anaitwa Dk. T. A Dar  alikuja Tanganyika mwaka 1930.
Mohammed Iqbal Dar alipata elimu yake ya msingi mkoani Morogoro katika Shule ya Msingi Aga Khan ambayo sasa ni shule ya serikali Mtwara na baada ya hapo alijiunga na Sekondari ya Mzumbe akasoma kidato cha kwanza mpaka cha sita.
Aliingiaje kwenye shindano la kupendekeza jina la Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar?
Mohammed anasema alikuwa Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam akijisoma gazeti la Tanganyika Standard (siku linaitwa Daily News) akaona tangazo linasema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unafahamika kama Republic of Tanganyika and Zanzibar jina lililoonekana refu sana kwa hiyo wananchi wote wakaombwa washiriki kwenye shindano la kupendekeza jina moja litakalozitaja nchi zote mbili yaani Tanganyika na Zanzibar.
Mohammed Iqbal Dar anasema aliamua kuandika jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Anasema kwanza alichukua karatasi akaandika Bismillah Raahman Rahimu hii ni kutokana na imani yake katika dini na baada ya hapo akaandika jina la Tanganyika kisha  akaandika Zanzibar halafu akaandika jina lake Iqbal.
Baada ya hapo  akaandika jina la Jumuiya yake ya Ahmadiya na baada ya hapo akamrudia tena Mwenyezi Mungu akamwomba amsaidie ili apate jina zuri kutoka katika majina hayo aliyokuwa ameyaandika.Lakini baada ya kumaliza kuandika hayo akajiuliza maswali mengi.

0 comments:

Chapisha Maoni