Jumatatu, Juni 09, 2014

SAKATA LA UBAKAJI, MBASHA VS GWAJIMA, MAPYA YAIBUKA

MUME wa mwimba Injili Bongo, Flora Mbasha anayedaiwa kumbaka binti wa miaka 17 (jina lipo), Emmanuel Mbasha ameibuka mzimamzima na kumtaka Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Uzima na Ufufuo la jijini Dar, Josephat  Gwajima amuachie mke wake, yaani Flora.

Akizungumza kwa machungu kwa njia ya simu kutokea alikojihifadhi huku akionesha waziwazi hasira juu ya hisia zake, Mbasha alisema:
Nimesika mke wangu baada ya matatizo yetu amehamia nyumbani kwa Gwajima. Nataka mumwambie Gwajima aniachie mke wangu, mbona ananifanyia hivyo?
KINACHOMSHANGAZA
Mbasha ambaye mpaka sasa hajulikani alipo, aliendelea kudai kwamba kinachomshangaza zaidi ni kwamba, Flora amekiuka utamaduni wa Kiafrika, kwamba kama mke na mume wamegombana kiasi cha kushindwa kuishi nyumba moja, mke anakwenda kwao lakini hilo la Flora kukimbilia kwa Gwajima ndilo la ajabu zaidi kwake.

Kama kweli Flora ameshindwa kuishi nyumbani kwetu (Tabata-Kimanga) kwa nini asiende Morogoro kwa mama yake. Au kwa nini asirudi Mwanza kwenye chimbuko la familia ya mzee Moses Kulola?
Yeye badala yake amechukuliwa na Gwajima na kwenda kuishi naye nyumbani kwake. Mimi sijapenda, sijapenda na sitapenda kamwe
alisema Mbasha.
ATUHUMU MTOTO KULIPIWA ADA YA SHULE
Akiendelea kutoa la moyoni, Mbasha alituhumu kuwa mke wake kwa sasa ana pesa nyingi licha ya kwamba wakati matatizo ya yeye kutuhumiwa kubaka yanatokea na kuingia mitini alimwacha hana kitu.
Anasema: 
Wakati matatizo yanatokea Flora nilimwacha mweupe. Mtoto wetu (Elizabeth) alitakiwa kupelekwa shule, kwa hiyo ina maana hakwenda.
Sasa nasikia mtoto amelipiwa ada na anakwenda shule. Nani kamlipia ada mwanangu kama si Gwajima? Mimi naumia sana, kwa nini iwe hivyo? Kama Gwajima ameamua mke wangu kukaa kwake kwa ajili ya kumsaidia kipindi hiki cha matatizio ajue mimi sijapenda.
Yeye Gwajima ana mke wake, najua hawezi kusema kitu kwa sababu Gwajima ni kila kitu lakini sijapenda.
GWAJIMA SASA
Jumamosi iliyopita, Uwazi lilimtafuta Mchungaji Gwajima kwa njia ya simu ambapo alisema hataweza kuzungumza kwa sababu yupo Mikumi akielekea Dar.
Chanzo: Sawa, lakini inadaiwa Flora yupo kwako. Hata jijini Dar habari zimeenea kwamba yupo kwako. Mbasha mwenyewe pia amesema mke wake yupo kwako. Unasemaje kuhusu hili?
Gwajima: Flora hakai kwangu na wala sijui alipo. Hao wanaosema anaishi kwangu si wa kweli. Hata mkija kwangu hamtamkuta Flora.

0 comments:

Chapisha Maoni