Jumamosi, Februari 11, 2017

17 WAFA UWANJANI ANGOLA

Kuna taarifa zimeripotiwa na mitandao mbalimbali duniani kuhusu vifo vya Watu 17 na  60 kujeruhiwa vibaya baada ya mkanyagano kwenye uwanja mmoja wa mpira nchini Angola.
Mkasa huo umetokea katika mji wa kazkazini mwa nchi hiyo Uige na taarifa hizo kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikiandamana na picha.
Mechi iliochezwa ilikuwa baina ya timu za Santa Rita de Cassia na Recreativo do Libolo,
Inadaiwa kitendo cha kundi la mamia ya watu la kuingia kwa nguvu kwenye uwanja huo ndio kilichosababisha mkasa huo.

0 comments:

Chapisha Maoni