Jumamosi, Februari 11, 2017

GWAJIMA AACHIWA, AZUNGUMZIA IBADA YA KESHO +VIDEO

Kiongozi wa kanisa la Ufufuo na Uzima la jijini Dar es alaam, Askofu Josephat Gwajima ameachiliwa leo kutoka katika mahabusu ya kituo cha kati cha polisi cha Dar es Salaam baada ya kushikiliwa kwa takribani masaa 48 tangu siku ya alhamisi aliposhikiliwa kwaajili ya mahojiano na jeshi la polisi.

Askofu Gwajima alishikiliwa na jeshi hilo kwa amri ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam aliyemtaja katika orodha ya pili ya watu waliohusishwa na matumizi au biashara ya madawa ya kulevya.

Baada ya kuachiwa kituoni hapo, Askofu Gwajima kupitia mitandao ya kijamii ameandika kuwa: 
 “FREE AT LAST: Mungu awabariki wote mlioomba kwa ajili ya jambo hili, kesho nitakuwepo kwa ajili ya Ibada ya Jumapili, Kanisa la Ufufuo na Uzima Dar es Salaam. Mungu awabariki sana nawapenda nawaombea wote mlioomba kwaajili ya hili”
Kesho ni siku ya jumapili, kama kiongozi wa kanisa hilo ameandika tena kwamba:
"Kesho nitakuwepo kwaajili ya Ibada ya Jumapili, Kanisa la Ufufuo na Uzima Dar es Salaam. Mungu awabariki sana nawapenda nawaombea wote mlioomba kwaajili ya Hili. I'm a #Heavenlyman" 

0 comments:

Chapisha Maoni