Jumamosi, Februari 11, 2017

SINGIDA UNITED YAPANDA LIGI KUU SOKA TANZANIA BARA

Kutoka ligi daraja la kwanza nchini Tanzania Bara, Timu ya Lipuli FC Wanapaluhengo kutoka mkoani Iringa tayari walikwisha jipatia nafasi ya kucheza ligi kuu soka Tanzania Bara kwa msimu ujao wa mwaka 2017/2018 baada ya ushindi wa 3-1 walioupata mara ya mwisho dhidi ya Polisi Dar es Salaam na kutwaa pointi ambao haziwezi fikiwa na timu yoyote katika kundi A.
Baada ya Lipuli kujihakikishia nafasi katika Ligi kuu msimu ujao, timu ya soka kutoka mkoani Singida, Singida United nayo imekata tiketi ya kucheza ligi kuu mshimu ujao hii leo baada ya kupata ushindi wa 2-0 dhidi ya Alliance School na kufikisha pointi 30 ambazo haziwezi fikiwa na timu yoyote katika kundi lake kutokana na Rhino Rangers kupata sare ya 2-2 na Panone.
Wakati hayo yakitokea, Lipuli FC leo wametoka sare tasa na timu ya Ashant United.

0 comments:

Chapisha Maoni