Jumamosi, Februari 11, 2017

ULINZI WA WANYAMA WAIMARISHWA TANZANIA NA KENYA

Ushirikiano imara kati ya Kenya na Tanzania katika uhifadhi wa wanyamapori, umetajwa kupunguza kwa kiasi kikubwa ujangili wa wanyamapori kama vile tembo na vifaru.
Wataalamu na wanaharakati walisema hayo katika mkutano wa Baraza la usalama wa wanyamapori la Kilimanjaro ulioandaliwa na Mfuko wa Wanyamapori wa Afrika AWF, ambao ulijadili mikakati ya uvumbuzi inayolenga kuimarisha uwezo wa kukabiliana na matishio dhidi ya wanyamapori katika kanda hiyo.
Mlinzi wa hifadhi ya wanyamapori ya Longido, Bw Peter Kapingwa amesema, wamefanikiwa kuzuia ujangili katika hifadhi za wanyamapori zinazotumiwa na pande mbili katika miaka minne iliyopita kutokana na ushirikiano wa kuvuka mpaka.
Walinzi wa wanyamapori wameimarisha juhudi za kulinda makundi yaliyosalia ya tembo na faru katika eneo la Kilimanjaro lililoko kwenye mpaka wa Kenya na Tanzania.

0 comments:

Chapisha Maoni