Hali ya simanzi
imetawala miongoni mwa wakazi wa Makete mjini mkoani Njombe kufuatia
utingo wa lori lililobeba skaveta kugongwa na lori hilo hadi kufa papo
hapo.
Tukio hilo limetokea
jana majira ya saa 11:45 alfajiri wakati lori hilo likipita kwenye eneo
lililolundikwa vifusi kufuatia matengenezo ya barabara hiyo kwa kiwango
cha lami.
Lori hilo lilikuwa likiendeshwa na Bw. Lewad Mekule ambaye kwa sasa anashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi na upelelezi tayari umekamilika hivyo atafikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya mauaji yanayomkabili.
Akizungumza na eddy
blog mkuu wa polisi wilaya ya Makete Bw. Alfred Kasonde amemtaja
marehemu kuwa ni Albert Mwalukasa (21) ambaye amegongwa na lori hilo
lenye namba za usajili T 489 BDW mali ya Timoth Mwalukasa mkazi wa mkoa
wa Mbeya.
Baba mdogo wa marehemu aitwaye Allan Mwalukasa ambaye alikuwepo kwenye lori hilo amesema hata yeye anashangaa kilichopelekea kifo cha ndugu yake kimetokeaje.
Nilikuwa mbele hapa naangalia sehemu ambayo kidogo ni nzuri kwa ajili ya vifusi hapa ambavyo vimelundikwa barabarani ghafla nkashangaa nimesikia kelele nyuma huko analia aaaaah nikashindwa kuelewa, kuja kukimbia ninamkuta yupo chini ya gari, huyo ni mtoto wa kaka yangu ambaye tumefuatana
amesema Mwalukasa.
Kwa upande wa wananchi waliofika eneo la tukio wamesema marehemu alikuwa akimuongoza dereva namna ya kupitisha lori kwenye vifusi vilivyolundikwa muda mrefu barabarani bila kusambazwa, lakini ghafla aliteleza kwa kuwa alikuwa akipita juu ya vifusi hivyo ndipo alipogongwa na kufariki papo hapo.
Wananchi hao wametupa lawama kutokana na vifusi hivyo kukaa muda mrefu bila kusambazwa hali inayopelekea usumbufu kwa watumiaji wa barabara hiyo, na hivi karibuni mwandishi wetu alizungumza na mkandarasi wa ujenzi huo ambaye alisema amekwenda Morogoro kufuata vifaa vya kumalilisha ujenzi huo.
Hata hivyo wameshauri barabara mbadala zilizojengwa na mkandarasi huyo zitumike ili kuepusha madhara zaidi.

0 comments:
Chapisha Maoni