Usiku wa kuamkia hii leo ulikuwa maalum katika historia ya
kuanza tena kwa michuano ya ligi ya barani Ulaya *Europa League* msimu
huu katika hatua ya makundi, ambapo klabu kadhaa za mataifa mbali mbali
barani humo zilipambana kwa lengo la kusaka point tatu muhimu.
Nchini Ujerumani wakati historia hiyo ikiandikwa, wenyeji Borussia
Monchengladbach walikuwa wakipambana na klabu Villarreal kutoka nchini
Hispania huko Stadion im Borussia-Park.
Katika mchezo huo ambao ulimalizika kwa sare ya bao moja kwa moja,
kiungo wa Borussia Monchengladbach, Granit Xhaka aliustaajisha ulimwengu
wa wapenda kandanda baada ya kukota simu katika sehemu ya kuchezea.
Kitendo cha mchezaji huyo kuokota simu uwanjani kilifanyika wakati
mpambano ukiendelea, hatua ambayo iliwalazimu wapiga picha kufuatilia
kwa ukaribu kwa kutaka kubaini ni nini kilichookotwa na Granit Xhaka.
Hata hivyo baada ya kuiokota simu hiyo, Granit Xhaka alipeleka moja
kwam moja kwa muamuzi wa mchezo huo, kwa ajili ya kupisha mambo mengine
yanayohusu mpambano huo kuendelea.
Lakini baada ya mchezo huo kumalizika mmoja wa maafisa wa benchi la
ufundi la klabu ya Monchengladbach, alidai simu hiyo ilikuwa ya kwake
lakini haikufahamika ni wakati gani aliiangusha uwanjani ama ilifika
vipi katika sehemu ya kuchezea.
0 comments:
Chapisha Maoni