Kundi la wasichana na wavulana sita wa Iran waliocheza wimbo wa
Pharrell Williams ‘Happy’ na kisha video yao kusambaa kwenye mitandao
mwezi May mwaka huu wamekamatwa tena rasmi na kuhukumiwa kifungo cha
miezi sita jela na bakora 91.
Hukumu hiyo inakuja ikiwa ni miezi kadhaa tangu walipokamatwa kwa
kosa hilo na kuachiwa kwa muda baada ya watu mbalimbali duniani kukemea
kwa nguvu kitendo hicho kwa kuwa waliamini vijana hao walikuwa
wanajifurahisha tu.
Hata hivyo, kitendo hicho kilitafsiriwa kuwa kinyume na sheria za
nchi hiyo hususani mavazi waliyokuwa wamevaa na aina ya michezo
waliyoicheza.
Vijana hao walikiri kosa hilo na kueleza kuwa walirubuniwa na watu
kuwa ilikuwa sehemu ya usaili wa kazi ya uigizaji jijini Tehran.
Muda mfupi baada ya hukumu hiyo kutajwa, mwanasheria wa aliyekuwa
anawatetea vijana hao, Farshid Rofugaran ameeleza kuwa hukumu hiyo
imesamehewa kwa mujibu wa sheria na kwamba itatekelezwa endapo vijana
hao watarudia kosa kama hilo ndani ya kipindi cha miaka mitatu.
0 comments:
Chapisha Maoni