Bunge Maalumu la Katiba la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha
azimio la kuzifanyia marekebisho kanuni za 30, 36 na 38 ili kuruhusu
wajumbe watakaokuwa nje ya Bunge iwe ndani au nje ya nchi, wapige kura
za kuamua ibara na sura za rasimu ya katiba popote watakapokuwa. Kwa
mabadiliko hayo, wajumbe wa Kiislamu waliokwenda kutekeleza ibada ya
Hija Makka Saudi Arabia, wanaopata matibabu nchini India na walio katika
majukumu mengine ndani na nje ya nchi, watapiga kura kuamua rasimu ya
katiba mpya inayopendekezwa. Hata hivyo mabadiliko hayo yalizua mjadala
na mvutano mkali kati ya Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta na
baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo maalumu la Katiba. Taarifa zaidi kutoka
ndani ya Bunge la Katiba zinasema kuwa, Septemba 25 wajumbe watakaa
kwenye kamati kuona kama mapendekezo yao yamewekwa ipasavyo kwenye
rasimu hiyo na baada ya hapo Septemba 27 na 28, kamati ya uandishi
itaiweka sawa rasimu hiyo ili Septemba 29 hadi Oktoba 2 mwaka huu,
ipigiwe kura.
0 comments:
Chapisha Maoni