Ripoti iliyotolewa kuhusu tenda ya kuhodhi michuano ya kombe la dunia
kwa mwaka 2018 na mwaka 2022 imeelezwa huenda ikasabisha wanaoshutumiwa
kufunguliwa mashtaka
Mbunge wa chama cha Conservative nchini uingereza, Damian Collins
aliitaka ofisi inayochunguza maswala ya udanganyifu na rushwa kuomba
nakala ya ripoti iliyotolewa kuhusu mchakato wa kutoa tenda kwa ajili ya
michuano ya kombe la dunia mwaka 2018 na 2022, akisema kuwa anaamini
Ripoti hiyo huenda inatoa ushahidi kuhusu madai ya vitendo vya rushwa.
Mwanasheria kutoka nchini Marekani, Michael Garcia alitoa ripoti yake
mwezi huu, lakini Fifa imesema yaliyomo kwenye ripoti hiyo hayatatolewa
hadharani
Kamati ya Qatar iliyokuwa ikiwania tenda kuhodhi michuano ya kombe la
dunia mwaka 2022 inakabiliwa na shutuma kuwa ilitoa rushwa kupatiwa
nafasi hiyo,baada ya Gazeti moja kuripoti mwezi juni kuwa aliyekuwa
makamu wa rais wa fifa Mohamed bin Hammam alitoa rushwa ya pauni milioni
tatu ili kupata tenda hiyo.madai ambayo Qatar imeyakanusha. Uamuzi baada ya kutoka kwa ripoti hiyo utatolewa mwakani.
0 comments:
Chapisha Maoni