Watafiti nchini Uingereza wanaofanya utafiti kuhusu
matumizi ya dawa ya Asprin kupunguza magonjwa, wanapendekeza kuwa watu
walio na umri wa zaidi ya miaka 50 wanapaswa kushauriana na daktari
kuhusu matumizi yake kila siku ya maisha yao.
Wanaamini kwamba dawa hiyo inaweza kupunguza idadi ya watu wanaopata Saratani hasa Tumboni.
Watafiti hao kutoka Chuo kikuu cha Queen Mary
jijini London, wanachunguza data zote zinazopatikana kielimu na
majaribio kadhaa ya kliniki iwapo dawa ya Aspirin ina uwezo wa kutibu
baadhi ya maradhi.
Wanasema kuwa ni jambo la busara kuweza
kukomesha baadhi ya vifo vinavyotokana na maradhi ya mshtuko wa Moyo au
kuvuja damu Tumboni.
0 comments:
Chapisha Maoni