Chile imemfuta kazi afisaa mkuu wa usalama katika
uwanja rasmi wa ndege baada ya tukio la kuaibisha la wizi wa zaidi ya
dola milioni kumi katika sehemu ya kupakia mizigo.
Waziri wa ulinzi George Burgos, amesema kuwa
uchunguzi umeanzishwa kuhusu namna wanaume 8 waliokuwa wamejihami kuiba
pesa kutoka kwa gari lenye ulinzi mkali katika uwanja wa ndege katika
mji mkuu Santiago.
Alitaja tukio hilo la Jumanne kama la kutia aibu na la kushangaza sana na linalostahili hatua kali.
Picha za video, zilionyesha genge hilo lililofanya kitendo chao kwa kujidai kuwa wafanyakazi wa uwanja wa ndege.
Wakati uchungizi unapoendelea, afisa mkuu wa usalama katika uwanja wa ndege, Arturo Merino Benitez Airport ameachishwa kazi
alisema bwana Burgos.
Pia aliahidi kwamba usalama utadhibitiwa katika uwanja huo na kufanyiwa mabadiliko makubwa.
Wezi waliingia katika sehemu ya kupakia mizigo
ya uwanja wa ndege wakiwa wamevalia nguo za kazi,na kulisimamisha gari
lililokuwa limebeba pesa hizo. Inaarifiwa gari hilo lilikuwa na ulinzi
mkali sana.
Pesa hizo zilikuwa zinaelekea katika benki na kampuni za migodi Kaskazini mwa Chile.
Wanaume hao waliwaondoa walianzi kwenye gari hilo na kuchukua pesa kabla ya kutoroka bila hata ya kufyatua risasi yoyote.
Kitendo chenyewe cha wizi ambacho ni kikubwa
sana katika historia ya Chile, hakikunaswa kwenye kamera za ulinzi,bali
walionekana wakitoroka.
0 comments:
Chapisha Maoni