Binafsi mie mwenyewe Mr. Fichuo nilikuwa natamani sana kuiona video ya 'PROKOTO' ambao ni wimbo wa Victoria Kimani, mwanadada mrembo kutoka nchini Kenya ambaye pia wakati wa kufanya wimbo huo aliingia katika mgogoro mkubwa na Wema Sepetu a.k.a baby wa Diamond Platnumz ambaye pia kashirikishwa katika wimbo huo ikidhahaniwa kuwa Diamond anachepuka na mkenya huyo...lakini kumbe walaaaa ni kazi tu!
Hatimaye sasa video ya wimbo huo iliyofanyika nchini Kenya imetoka na nikukumbushe pia video hii ilimwingiza Ommy Dimpoz ambaye pia kashirikishwa ndani ya wimbo huo katika Beef ndogo na Victoria Kimani baada ya PKP kudai kuwa hawezi fanya kazi tena na madirector kutoka nchini Kenya kwasababu tayari amepiga hatua na kufanya kazi na madirector kutoka nchini Nigeria mpaka pale Victoria kimani alipotishia kuwaataitisha mkutano na waandishi wa habari wa Kenya (Press Comference) ili kutangaza kashfa hiyo na hapo ndipo Dimpoz akatulia na kufanya kazi.
Itazame hapa Prokoto-Victoria Kimani ft. Diamond Platnumz & Ommy Dimpoz
0 comments:
Chapisha Maoni