Wajumbe kutoka shirika la afya ulimwenguni wanakutana
Geneva Uswis kuamua iwapo wautangaze mlipuko wa ugonjwa wa Ebola kama
janga la barani Afrika na dharura ya dunia. Mkutano huo unakuja wakati raia mmoja wa Saudia Arabia amefariki akiwa na dalili za ebola katika mji wa Jeddah.
Iwapo itathibitika msaudia huyo
amekufa kwa ebola, kitakuwa kifo cha kwanza nje ya bara la Afrika
kusababishwa na virusi vya Ebola. Arnold Kayanda na maelezo zaidi.
Tayari ugonjwa huo ambao umeenea zaidi katika
eneo la Magharibi mwa Afrika umeshaua zaidi ya watu 900 kwa mwaka huu na
unaonekana kuenea kwa kasi katika maeneo mengine baraani humo.
Vifo hivyo pamoja kasi ya kuambukiza huenda
ikiwa kichocheo cha kulifanya shirika la Afya duniani kutangaza ugonjwa
huo kuwa janga na dharura ya dunia.
Dr Ben Newman mtafiti wa masuala ya virusi
katika chuo kikuu cha Reading anasema kuitangaza Ebola kama dharura ya
dunia itasaidia
"Kama itakubalika hali hii kutangazwa kama
suala la dharura itawaruhusu kuingia nchini na itawaruhusu kutoa msaada.
Msaada kwa maana ya watu, usalama wa madaktari, na itawaruhusu kutoa
misaada ya kifedha. Hiyo ni muhimu kwa sababu miundo mbinu katika baadhi
ya maeneo yenye virusi haitoshi" amesema Dr Newmana.
Mbali na kutangaza ebola kuwa hali ya dharura
pia shirika hilo la Afya duniani limesema kuwa mapema wiki ijayo
litakuwa na mkutano wa wataalamu wa maadili ya afya kujadili uwezekano
wa kutumia matibabu ya majaribio ili kudhibiti Ebola.
Tamko hilo linakuja kufuatia wamarekani wawili
walioathirika na Ebola kupewa dawa hiyo 'Zmapp' na kuonekana kupata
nafuu. Dr Derek Gatherer mkufunzi katika chuo kikuu cha Lancaster
amesema maamuzi juu ya matumizi ya dawa ya majaribio huenda yakawa
magumu.
0 comments:
Chapisha Maoni