Kwanza ifahamike Nigeria kuna watu zaidi ya Mil170 na Tanzania ni kama
watu Mil44 hivi kwa harakaharaka na hatutaweza hata robo kushindana nao
sababu hawa jamaa kwanza wanashinda katika internet. Watumiaji wa
Internet Tanzania ni asilimia haizidi 4 au 5. Hatufiki watu mil1 na nusu
na wengi wanaotumia wako nje ya Tanzania na
Miji Mikubwa sana. Ndio maana kama una biashara yako ya maana Tangaza
radioni sababu watu mil44 wote karibia wana Access ya radio. Mtu yoyote
afanyaye kazi kwenye media ni Maarufu zaidi ya hawa wa instagram
facebook au twitter au bloggerz au wanaomiliki blogs. Sababu hao watu
mil44 ni lazima watamfahamu tu. Pili uki shoot video na Jamaa wa Nigeria
wanaichukua na kukutambulisha duniani wenyewe kupitia ile pesa yako na
sio kuwa wewe ndio eti unasumbuka hapana. Na sio kuwa ukichaguliwa BET
au sijui wapu ni Nguvu zako hapana ni hao Jamaa wanafanya hayo yote.
Nawashauri Wasanii wenye uwezo wa kufanya video na watu wa Nigeria
wafanye hivyo na Matunda yao watayaona. They gon make you famous
Hutaamini. Wanasambaza kazi zako wenyewe kupitia Pesa yako uliolipa
wakati una shoot video. Adam Juma did it Mwanzo pia...so Nashauri wa
Tanzania tuwekeza katika video Nje za Nchi kama unataka Kutangaza nchi
na kuchaguliwa kwenye awards kubwa duniani. Nigeria pia Elimu
inachangia. Hawa watu wanaongoza kwa mengi duniani ikiwemo wizi wa ki
electroniki pia. So ndio maana wanashinda ma tuzo ma nini....akili
nyingi....degree na masterz kibao huko. Wasanii Tanzania pia ongezeni
Elimu zenu itawasaidia zaidi ....
0 comments:
Chapisha Maoni