Mtu mmoja mjini Alabama nchini Marekani amefungua kesi ya madai baada ya
kudai kuwa alikwenda kutahiriwa lakini madaktari wakaondoa uume wake
wote.
Tovuti ya Metro imesema Johnny Lee Banks Jnr anadai kuwa alikwenda kufanya 'suna' katika hospitali ya Princeton Baptist Medical Center na uume wake kukatwa kimakosa na madaktari.
Tovuti ya Metro imesema Johnny Lee Banks Jnr anadai kuwa alikwenda kufanya 'suna' katika hospitali ya Princeton Baptist Medical Center na uume wake kukatwa kimakosa na madaktari.
Kesi hiyo iliyofunguliwa na Bwana Banks pamoja na mkewe Zelda, inasema bwana huyo hakupewa maelezo yoyote
ya kwanini 'mashine' yake iliondolewa na wala hakuonywa kuwa shughuli
ya kutahiri ina hatari na uwezekano wa kukatwa kabisa uume.
Mshtaki alipozinduka kutoka kwenye dawa ya usingizi baada ya upasuaji, alikuta uume umekatwa
yamesema maelezo ya mashtaka.
Mdai hakutoa idhini yoyote ya kukata kabisa au nusu ya uume wake
imesema karatasi ya mashtaka.
Bwana huyo ameitaja hospitali, pamoja na madaktari wawili kuwa ndio washtakiwa katika kesi hiyo, akisema walikuwa wazembe na walishindwa kutafuta msaada walipopatwa na tatizo wakati wa upasuaji.
Bwana huyo ameitaja hospitali, pamoja na madaktari wawili kuwa ndio washtakiwa katika kesi hiyo, akisema walikuwa wazembe na walishindwa kutafuta msaada walipopatwa na tatizo wakati wa upasuaji.
0 comments:
Chapisha Maoni