Jumatano, Julai 30, 2014

MAN UTD YAICHAPA INTER MILAN 5-3

KOCHA Louis van Gaal ameendeleza wimbi la ushindi baada ya Manchester United kuifunga Inter Milan kwa penalti 5-3 kufuatia safe ya 0-0 katika mchezo wa Kombe la Kimataifa kujiandaa na msimu mpya nchini Marekani.
Katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa FedEx Field mjini Washington, penalti za United zilitiwa nyavuni na Ashley Young, Javier Hernandez, Tom Cleverley, Shinji Kagawa na Darren Fletcher wakati Marco Andreolli wa Inter aligongesha mwamba. Van Gaal akipanga vikosi viwili, kimoja kila kipindi.
Man United kipindi cha kwanza: Lindegaard, Smalling, Jones, Evans, Valencia, Fletcher, Herrera, Young, Mata, Rooney, Welbeck
Kipindi cha pili: De Gea; M Keane, Evans, Blackett; Young, Cleverley, Fletcher, Kagawa, Shaw; Zaha, Nani/Hernandez dk77.
Inter Milan: Handanovic/Carrizo dk63, Ranocchia, Vidic/Andreolli dk72, Juan Jesus, D'Ambrosio, Jonathan, Kuzmanovic/Laxalt dk63, Krhin/M'Vila dk46, Dodo/Nagatomo dk63, Botta/Taider dk63 na Icardi.

0 comments:

Chapisha Maoni