Jumatano, Julai 30, 2014

TETESI ZA SOKA ULAYA

Beki was Aston Villa Ron Vlaar, 29, atakuwa na mazungumzo na meneja wake Paul Lambert kuhusiana na hatma yake licha ya Southampton kumwania (Daily Mirror), QPR wanafikiria kumchukua kiungo wa Colombia Carlos Sanchez, 28, kwa pauni milioni 4 kutoka Elche (Daily Mirror), West Ham na QPR wamepanda dau kwa Marseille kumchukua Matheiu Valbuena baada ya kiungo huyo Mfaransa kukataa kuhamia Dynamo Moscow (L'Equipe), Manchester United na Barcelona bado wanamfuatilia Juan Cuadrado, 26, wa Fiorentina lakini huenda wakatishwa na bei ya pauni milioni, 32, ya kiungo huyo kutoka Colombia (Marca), Manchester United wamefikia makubaliano "ya mdomo" na kiungo wa Juventus Arturo Vidal, 27, ya uhamisho wa pauni milioni 47 (Tuttosport), matumaini ya Manchester City kumsajili beki kutoka Morocco Mehdi Benatia, 27, yamefifia baada ya Roma kusema hakuna dalili za mchezaji huyo kuondoka (Le Figaro), meneja mpya wa Manchester United amewaonya mashabiki wake kuwa timu hiyo huenda ikasuasua katika miezi mitatu ya mwanzo wa msimu wakati wachezaji wakianza kuzoea mbinu zake (Times), Van Gaal amesema iwapo watashinda Ligi Kuu msimu ujao na kuwapiku majirani zao Manchester City, utakuwa ushindi "mtamu" zaidi (Manchester Evening News), kiungo wa Manchester City Yaya Toure, 31, amesema huenda akasalia katika timu hiyo hadi atakapoacha kucheza soka (Guardian), mshambuliaji mpya wa Barcelona Luis Suarez, 27, ambaye anatumikia adhabu ya miezi minne, amehamia katika mji wa Pyrenees kuanza mazoezi ya msimu mpya akiwa na mwalimu binafsi (Daily Mail), Didier Drogba, 36, amesema Diego Costa, 25, atakuwa mchezaji "mkali" katika Ligi Kuu ya England (Sun), AC Milan wanafanya mazungumzo wa mshambuliaji kutoka Brazil Robinho, 30 (Le Figaro), kiungo wa Arsenal Santi Cazorla,29, bado anasakwa na Atlètico Madrid. Atlètico pia wanamfuatilia Fernando Torres, 30, na winga wa PSV Eindhoven Zakaria Bakkali, 18 (AS.com), kiungo anayefuatiliwa na Liverpool, Xeridan Shaqiri, 22, huenda akaamua kubakia na klabu yake ya Bayern Munich (Tuttosport), Borussia Dortmund na Schalke wanamtaka mshambuliaji kutoka Serbia, Aden Ljajic, 22, kutoka AS Roma (Bild), Barcelona wametangaza kumsajili kiungo kutoka Brazil, Alex Varoneze Dione anayejulikana kama "Betri" kwa miaka mitatu (Mundodeportivo), Manchester United wameanza tena kumfuatilia beki wa kati wa Atletico Madrid Miranda, baada ya Atlètico kusema wapo tayari kupokea dau la pauni milioni 23 (Metro), AC Milan wanamtaka winga wa Newcastle Hatem Ben Arfa na huenda akauzwa kwa pauni milioni 12 (Daily Star), Bayern Munich wapo tayari kusubiri hadi Oktoba kumsajili kipa wa zamani wa Barcelona Victor Valdez ambaye anauguza jeraha la goti, ingawa anaweza kusita kwenda kugombea namba na Manuel Neuer (Mundo Deportivo), QPR wanataka kumchukua Ronaldinho ambaye amemaliza mkataba wake na Atletico Mineiro (Globoesporte) na Chelsea wanakataa kutengeneza jezi zenye jina la kipa Thibaut Courtois, 22 na Romelu Lukaku, 22, kwa sababu wachezaji hao bado hawajapewa namba (Daily Star).

0 comments:

Chapisha Maoni