Jumatano, Juni 11, 2014

WASANII WAMWALIKA RAIS KWENYE UZINDUZI WA KAMPENI YA NAIAMINIA TANZANIA

Naiminia Tanzania ndiyo habari ya mjini, weekend hii, siku ya Jumamosi ndani ya uwanja wa Jamhuri, Mkoani Dodoma wasanii wa fani mbalimbali hapa nchini wameandaa ufunguzi wa kampeni kubwa inayoitwa ‘Naiaminia Tanzania’.
Ambayo ni muendelezo wa ile ngoma yao ya Miaka 50 ya Tanzania, wali irecord wasanii 50, wakashoot na Video, Mwana Fa pamoja na Nikki wa Pili watatoa speech mbele ya mgeni rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Dr Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dr Shein, atakuwepo Waziri Mkuu, Mh Mizengo Pinda pamoja na Baraza la Mawaziri na viongozi mbalimbali.
Pale Jamhuri Stadium kuzama itakua free bila mtonyo ili raia wote wapate chakula cha ubongo kwa watakao kua nje ya Dodoma wataweza kuona.

0 comments:

Chapisha Maoni