Achana na Maalim Hassan, safari hii ameibuka Nabii wa Huduma ya Ufufuo
iliyopo Buza jijini Dar es Salaam, Yaspi Paul Bendera (pichani) ambaye
amekazia kuwa vifo kwa wasanii wa Kibongo vitaendelea.
Akizungumza bila Nabii Bendera alisema:
Nimeona kwamba, ndani ya mwezi huu (Juni) watakufa wasanii 20. Huu si utani, ni maono.
Hakuna masharti magumu, Mungu anawapenda wasanii, lakini ikiwa wanataka kuepukana na vifo ninavyoviona mimi, waje kanisani kwangu niwapake mafuta matakatifu.
Wanatakiwa kumgeukia Mungu sasa, hali siyo nzuri. Nasisitiza waje niwapake mafuta matakatifu, vinginevyo wataendelea kupukutika.
Nabii huyo aliendelea:
Kuna msanii mmoja anasali kanisani kwangu, anaitwa Herieth (Chumila). Nilimpa huu ujumbe awafikishie wenzake. Anayepuuza na apuuze lakini nawahakikishia wakimgeukia Mungu haya mabalaa hayatawakumba kamwe.
Baada ya hayo naye Herieth ‘Mama wa Bongo Muvi’ athibitisha kuwa kweli alipewa ujumbe huo na Nabii Bendera awafikishie
wenzake.
Ni kweli nasali pale, ni kweli pia nilitumwa na Nabii Bendera nikazungumze na wasanii wenzangu kuhusiana na maono aliyooneshwa.Naamini utabiri wake kwa sababu nasali pale na siku aliyotabiri mambo hayo ndiyo siku aliyofariki dunia Mzee Small, nawashauri wasanii wafuate ushauri huo, waende tu kwani wakipakwa mafuta hayatawadhuru kwa lolote kwa sababu amekuwa akitabiri mambo mengi na yametokea
alisema
Mama wa Bongo Muvi.
Licha ya utabiri huo wa aina yake wa Nabii Bendera, mchungaji mmoja
wa makanisa ya kiroho ambaye hakupenda jina lake liandikwe mtandaoni kwa
kuhofia malumbano alipingana na utabiri huo akisema ni gia ya kutafutia
waumini.
Hakuna kitu kama hicho. Aseme anataka kupata waumini wengi. Kama kweli yeye alioneshwa hayo maono kwa nini asiishie kuwaombea tu? Kwa nini amesema waende kanisani kwake akawapake mafuta na asiwaelekeze waende kwenye makanisa yaliyo karibu nao?Huyo anataka waumini, asidanganye watu. Mungu ninayemwamini anaishi ndani ya nafsi ya mtu. Kama kweli aliona hayo, dawa yake yalikuwa maombi tu, siyo kwenda kupakwa mafuta, tena na yeye mwenyewe
alisema
mchungaji huyo.
0 comments:
Chapisha Maoni