Alhamisi, Juni 12, 2014

MAREKANI KUISAIDIA IRAQ

Rais Barak Obama amesema anaangalia uwezekano wa kutumia njia mbali mbali za kuisaidia Iraq kukabiliana na mashambulizi wanamgambo wa kiislam wanadhibiti eneo kubwa la kaskazini mwa Iraq .
Hata hivyo maafisa wa Marekani wamesema wanaendelea na majadiliano ili kuona kama vikosi vya kijeshi katika taifa.
Nchini Iraq kwenyewe wanamgambo hao wamepata udhibiti zaidi mashariki mwa jimbo la Diyala, lakini mashambulizi ya anga ya vikosi vya serikali yameelezekwa magharibi zaidi eneo la Samara.
Katibu wa NATO Anders Fogh Rasmussen amesema hali hiyo haivumiliki juu ya vitendo dhidi ya wanamgambo hao wa kiislam japo amesema kuwa Iraq yenyewe inapaswa kutafuta namna ya mgogoro huo.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani Jen Psaki ametoa ufafanuzi akidai kuwa watalaam wao bado wanaendelea na majadiliano na kwamba si nia ya nchi yake kurejesha vikosi vyake Iraq japo kuwa inaona haja ya kutoa msaada kwa nchi hiyo kutokomeza makundi hayo.

0 comments:

Chapisha Maoni