Jumanne, Juni 10, 2014

UN WATOA BARAKA KWA KOMBE LA DUNIA


Umoja wa Mataifa umeandaa sherehe maalumu kwa lengo la kuzikaribisha fainali za Kombe la Dunia la soka zitakazoanza kesho kutwa nchini Brazil.
Akihutubia kwenye hafla hiyo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon akiwa pamoja na wawakilishi kutoka nchi 32 zinazoshiriki kwenye fainali hizo, alisema kwamba mchezo wa soka una washabiki wengi hivyo unaweza kusaidia katika kuimarisha usalama na amani duniani. Ban Ki moon ameongeza kuwa, michezo licha ya kuwa na faida kwa mtu binafsi, inachangia katika kuleta umoja na mshikamano katika jamii ya mwanadamu. Amesisitiza kwamba fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil ni fursa nzuri ya kukidhi mahitajio ya mwanadamu yaani umoja na mshikamano.
Mwakilishi wa Iran kwenye sherehe hizo Rashid Bayat Mukhtari ameitakia mafanikio makubwa timu ya taifa ya soka ya Iran na kuyataja mashindano hayo kuwa ni nembo ya umoja na mshikamano wa mataifa yote ulimwenguni.
Fainali za Kombe la Dunia zinatarajiwa kutimua vumbi kesho kutwa, kwa pambano la ufunguzi kati ya wenyeji Brazil na Croatia.

0 comments:

Chapisha Maoni