Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini leo atakutana na kufanya
mazungumzo na Riek Machar, kiongozi wa wanamgambo waasi nchini humo huko
Addis Ababa, Ethiopia, ikiwa ni katika juhudi za kukomesha vita
vilivyodumu kwa miezi sita nchini humo.
Inatarajiwa kuwa, viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Kieneo ya
Mashariki mwa Afrika IGAD watashiriki kwenye mazungumzo hayo. Hii ni
mara ya kwanza kwa viongozi hao hasimu kukutana tokea yalipotiwa saini
makubaliano ya kusimamisha vita yaliyofikiwa tarehe 9 mwezi uliopita.
Mgogoro wa nchi hiyo uliingia kwenye hatua mpya baada ya pande hizo
mbili kukiuka mara kwa mara makubaliano ya usitishaji vita.
Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, hadi sasa maelfu ya watu
wameuawa na zaidi ya watu milioni moja na laki tatu wamelazimika kuwa
wakimbizi ndani na nje ya Sudan Kusini.
0 comments:
Chapisha Maoni