Swala la kubadili rangi ya ngozi limekuwa kama
msumari moto, kunao wanaoliunga mkono na wale wanaolipinga swala hilo
katu hawawezi kulifanya.
Baadhi wanasema kuwa ni wanawake wasiojithamini pekee ndio wenye kujichubua ngozi.
Mjadala huo ukiendelea, wasichana
wengi wanajitafutia umaarufu sio Marekani na Uingereza tu bali hata
katika kanda ya Afrika ya Mashariki. Wasichana hao wamekuwa wakifanya
kila wawezalo ela kupata huo umaarufu.
Mmoja wa wasichana hao ni Vera Sidika
anayejulikana sana nchini Kenya na afrika mashariki kwa kuwa na makalio
makubwa ambayo ndiyo yaliyompa umaarufu wake baada ya kuonekana katika
wimbo mmoja wa video uitwao 'You Guy' ambao baadaye ulipigwa marufuku
nchini Kenya.
Vera amejizidishia umaarufu kwa kubadili rangi yake ya ngozi, zamani
kidogo akiwa mweusi na sasa amejichubua na kuwa mweupe na pia kuwaambia
watu kuwa kubadili rangi ya ngozi yake ni yeye mwenyewe kujitakia. Hiyo
isiwashughulishe watu.
Vera anajulikana kwa kuwa na mazoea ya kujipiga
picha hasa za makalio yake na kuziweka kwenye mitandao ya kijamii. Vara
analinganishwa sana na Kim Kardhashian hasa kwa sababu ya umbo lake.
Kazi ya Vera hasa ni ya uwanamitido lakini mbali
na hilo Vera hulipwa ili kufika kwenye karamu mbali mbali , kwenye
disco na katika hafla mbali mbali za watu mashuhuri. Yeye pia hulipwa
kuwa katika kanda za video za wanamuziki maarufu Afrika Mashariki.
Alifichua kupitia televisheni Ijumaa kuwa alitumia maelfu ya dola kubadili rangi ya ngozi yake na kujifanya mweupe.
Shughuli hiyo aliifanyia nchini Uingereza na
ilimgharimu karibu milioni 15 pesa za Kenya, hizo ni dola 170,000 na
kwamba tayari kuna watu wengi wanaotaka sana kujichubua ngozi na
kufanana na Vera, kwa mujibu wa mwanadada huyo.
Vera anasema kuwa watu wamemsema sana kwenye mitandao ya kijamii
vibaya kwa sababu ya anavyoendesha maisha yake. Amewataja kama wanafiki
kwa sababu anasema huku wakiendelea kumsema na kumkosoa kwa kujichubua,
wamekuwa wakimuuliza alichofanya ili na wao watafute pesa wakafanye
hivyo kwa wanataka sana kufanan naye.
Mtindo wa wanawake kujichubua ni swala tata
nchini Kenya. Sio kama India ambako vipodozi vya kujichubua huuzwa wazi
wazi. Nchini Kenya bidhaa hizo, huuzwa kimagendo.
Wataalamu wanasema, wanawake wengi wanaendelea kujichubua licha ya hatari za bidhaa zinazouzwa kimagendo.
Swala la wanawake kijichubua barani Afrika
lilianza kujadiliwa waziwazi pale ambapo msanii raia wa Cameroon Dencia
kuzindua rasmi bidhaa zake za kuchubua ngozi ziitwazo, Whitenicious.
0 comments:
Chapisha Maoni