Jumapili, Juni 08, 2014

TETESI ZA USAJILI KATIKA MAGAZETI YA UINGEREZA LEO

Manchester United wamerejea tena kumfuatilia kiungo wao wa zamani Paul Pogba, anayechezea mabingwa wa Italia, Juventus- ambaye bei yake sasa ni takriban pauni milioni 60 (Sunday Express), Didier Drogba huenda akarejea Chelsea kutoka Galatasaray ya Uturuki (Sunday Mirror), Southampton watafanya mazungumzo wiki ijayo na Ronald Koeman ambaye huenda akachukua nafasi ya Mauricio Pochettino (Mail on Sunday), Manchester City watalipa pauni milioni 25 kumpata beki wa Real Madrid Pepe, ili kusaidiana na Vincent Kompany (Daily Star Sunday), Meneja wa Man United, Louis van Gaal amezungumzia kupendezwa na Arturo Vidal, na kukiri kuwa ni mchezaji ambaye "angependa kumnunua". Vidal kutoka Chile anayechezea Juventus, anasakwa na timu kadhaa ikiwemo Real Madrid, Barcelona na Chelsea (Mail on Sunday), Arsenal wanatazamia kumsaini tena Carlos Vela kutoka Real Sociedad kwa pauni milioni 3.25 (Sunday Sun), Arsenal pia wanamtazama kipa wa Nice, David Ospina, na huenda wakamfuatilia, lakini itategemea kiwango atakachoonesha wakati wa Kombe la Dunia (Sunday Mirror) Real Madrid watatazama dau kuanzia pauni milioni 40 kwenda juu kwa Angel Di Maria. Manchester United na Arsenal zinamtamani mchezaji huyo kutoka Argentina (L'Equipe), Paris St-Germain wanatazamia kuwazidi kete Arsenal, Liverpool na Manchester United katika kumsajili Antoine Griezmann, baada ya Eden Hazard kuhakikisha kuwa haondoki Chelsea (Daily Star) Carlos Vela ameiambia klabu yake ya Real Sociedad kuwa amepata mkataba mnono kutoka Atlètico Madrid (Marca). Share tetesi hizi na wapenzi wote wa kandanda. Tetesi nyingine kesho, tukijaaliwa.

0 comments:

Chapisha Maoni