Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger anafikiria kumsaini striker wa AC Milan
Mario Balotelli baada ya mchezaji huyo kuambiwa hahitajiki tena San
Siro (Daily Mirror), Liverpool, Chelsea na Tottenham pia zinaweza
kumfuatilia Balotelli (Daily Express), Arsenal wametupilia mbali nafasi
ya kumsajili tena Cesc Fabregas, licha ya kuwa Barcelona wapo tayari
kumuuza kwa pauni milioni 30 (Daily Mail), Manchester City ndio klabu
inayoonekana inataka kumchukua Fabregas,
huku Liverpool nayo ikimfuatilia, lakini Man United wako kimya ingawa
walimtaka sana msimu uliopita (Daily Mirror), Juhudi za Liverpool
kumsajili Adam Lallana zinasuasua baada ya Southampton kugoma kushusha
bei ya pauni milioni 30 (Times), mazungumzo ya mkataba kati ya Chelsea
na Frank Lampard yamegonga mwamba (Daili Express), Manchester City
huenda wakampa Lampard mkataba mfupi kabla ya kuhamia Marekani katika
klabu inayomilikiwa na City (Daily Mirror), Inter Milan inamtaka striker
wa Man U, Javier Hernandez "Chicharito" kwa mkopo.
Inter pia inamtaka
Fernando Torres (Daily Mail), Swansea wamekubali kulipa pauni milioni
6.5 kumsajili mshambuliaji wa FC Twente, Luc Castaignos (Sky Sports),
Liverpool wanakaribia kukamilisha usajili wa beki wa kushoto kutoka
Spain Alberto Moreno (Daily Mirror), nahodha wa Swansea Ashely Williams
yuko tayari kuhamia QPR (Daily Mail), Liverpool, Tottenham na Manchester
United wanamfuatilia beki wa Feyenoord Stefan de Vrij (Daily Star),
striker wa Spain David Villa ameondoka Atlètico Madrid na kuelekea New
York, Marekani (Sun), kiungo wa Ufaransa Franck Ribery huenda akakosa
kucheza Kombe la Dunia kutokana na majeraha ya mgongo (Metro) na
Manchester City hatimaye wanatarajia kukamilisha usajili wa kiungo
Fernando kutoka Porto kwa pauni milioni 12.2.
0 comments:
Chapisha Maoni