Jumatatu, Juni 02, 2014

MUSEVENI: NITAPELEKA VITHIBITISHO WA UADILIFU KWA PAPA ILI NYERERE ATANGAZWE MTAKATIFU

Rais Yoweri Museveni, amesema kiongozi bora ni yule anayefuata maagizo ya Mungu na kuwatumikia binadamu wote kwa usawa na haki.
Rais Museveni aliyasema hayo jana wakati wa ibada ya kuombea mchakato wa kumfanya Marehemu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kuwa mwenyeheri na hatimaye kutangazwa mtakatifu.



Alisema hata kwenye maandiko matakatifu ya Biblia kuna mistari inayomtaka binadamu ampende binadamu mwenzake kama anavyojipenda yeye;
Kwenye biblia kuna sehemu inauliza kuwa utampendaje Mungu ambaye hujawahi kumuona, na ushindwe kumpenda binadamu mwenzako
Alisema kwa sababu aliwahi kufanya kazi na Mwalimu, anaweza kutoa ushahidi kwamba Mwalimu alifanya yote mawili, kumtii Mungu na kuwatumikia binadamu.
Alisema mojawapo ya sababu iliyomfanya Marehemu Papa Paulo II kutangazwa mtakatifu kuisaidia Ulaya Mashariki, ambayo wananchi wake walikuwa hawamwamini Mungu.
Marehemu Papa Paulo II alisaidia kuikomboa Ulaya Mashariki kutoka kwenye ukomunisti, wananchi walikuwa hawaamini kuna Mungu, lakini kwa juhudi zake aliwafanya wamwamini na kumpenda Mungu
alisema.
Rais Museveni alisema anatarajia kupeleka ushahidi kwa Papa Francis kwamba Mwalimu anasifa za kutangazwa kuwa mtakatifu kwa sababu alimtii Mungu na kuwatumikia binadamu.
Mimi nitapeleka ushahidi kwa Papa, kwamba mbali na mwalimu kumtii Mungu na kuwapenda binadamu wote, pia aliwakomboa Waafrika kutoka Ruvuma mpaka Capetown, huu ni ukweli siyo hadithi
alisisitiza Rais Museveni.
Kufuatia hatua hiyo ya kwenda Roma kutoa ushahidi, Rais Museveni amesema katika maadhimisho ya kuombea mchakato wa Mwalimu kuwa Mtakatifu yatakayofanyika mwakani, ameahidi kuwaita maraisi wote waliowahi kufanya kazi na Mwalimu Nyerere ili kuuthibitishia ulimwengu kuwa Marehemu Baba wa Taifa ameweza kuwaunganisha Waafrika.

0 comments:

Chapisha Maoni